Saturday, February 22, 2014



CHANGAMOTO YA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA

Ukosefu wa njia za kupitisha wagonjwa  ndani ya hospitali ya Mkoa wa Mbeya, umesababisha wagonjwa na miili ya marehemu kubebwa mgongoni.

Hospitali hiyo ambayo ilijengwa kwa  kupitia michango ya wananchi na baadaye serikali kuitengea fedha  lakini bado zipo changamoto ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Akizungumza jijini mbeya  Katibu wa Hospitali hiyoDkt, Fanuel Mwasongela, alisema kukosekana kwa njia za kupitisha wagonjwa kunaleta shida na adha kubwa kwa wagonjwa,ndugu na watoa huduma.

Wagonjwa waliozidiwa wafikapo hospitali, hulazimika kubebwa mgongoni au kwa mikono toka yanapoegeshwa magari hadi vyumba vya madaktari ,  wodini na kwenye sehemu za uchunguzi kama vile chumba cha X-ray na mazoezi,”alisema

Amesema, pia adha hiyo imekuwa ikiwapata watoa huduma na ndugu wa miili ya marehemu kwa kubeba maiti hizo kwa kutumia mikono au mgongoni kutoka wodini hadi kwenye chumba cha kuhifadhia.

Aidha, Katibu huyo aliongeza kuwa mbali na tatizo hilo pia hospitali hiyo inakabiliwa  na upungufu mkubwa kwenye jengo la huduma za kina mama na watoto.

Amesema, mpaka sasa jengo hilo ni dogo na kwamba linavuja kiasi kwamba wagonjwa hulazimika kuhama toka baadhi ya vyumba huku vyumba vya upasuaji mdogo na mkubwa vikihitaji marekebisho ya haraka kwa usalama wa wagonjwa.

Hata hivyo, amesema kutokana na changamoto hiyo hospitali inahitaji shilingi milioni 500,000,000/= ili kufanikisha ukarabati wa jengo la huduma za mama na mtoto pamoja  na kujenga njia za kupitisha wagonjwa.

0 Responses to “ ”

Post a Comment

More to Read