Saturday, October 29, 2016
JAJI LUBUVA ATAKA TUMEYA UCHAGUZI IFUMULIWE..APENDEKEZAWAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAWEKWE KANDO KWENYE USIMAMIZI
Do you like this story?
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva ameitaka
serikali kubadili muundo wa tume hiyo ili iwe na ofisi na watumishi katika kila
halmashauri nchini na ofisi ya Zanzibar.
Amesema
hatua hiyo itawezesha NEC kufanya kazi zake kwa uhuru zaidi, badala ya
kutegemea wakurugenzi wa halmashauri (Ma-DED).
Alisema
hayo jana mjini Dodoma wakati akikabidhi taarifa ya tathimini baada ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,
Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Tathimini
hiyo imetolewa ikiwa ni mwaka mmoja tangu Rais wa Awamu ya Tano, Dk John
Magufuli kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo.
Lubuva
alisema serikali ifanyie mapitio ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 na
Sheria ya Serikali za Mitaa Sura 292 ili kurekebisha vifungu vinavyokinzana.
“Pamoja
na hayo, serikali inatakiwa kubadili muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili
kuwa na ofisi na watumishi katika kila halmashauri nchini na ofisi ya Zanzibar,
hiyo itafanya tume ifanye kazi zake kwa uhuru zaidi tofauti na sasa kazi hizo
zimekuwa zikifanywa na wakurugenzi wa halmashauri,” alisema.
Alisema
baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, tume iliamua kufanya tathimini kwa lengo
la kupata mrejesho juu ya utekelezaji wa Uchaguzi Mkuu kutoka kwa wadau.
Alisema ni mara ya kwanza kwa tume kufanya tathimini tangu kuanzishwa kwake
mwaka 1993.
“Tathimini
hii imefanyika ikiwa ni mojawapo ya zoezi linalokamilisha mzunguko wa uchaguzi
na kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mwingine,” alisema.
Alisema
changamoto zilizojitokeza kwa mujibu wa wadau waliohojiwa ni pamoja na mpiga
kura kutoruhusiwa kupiga kura katika eneo tofauti na lile alilojiandikisha.
Pia
wapiga kura kushindwa kupiga kura siku ya uchaguzi kutokana na kugawa mipaka ya
kiutawala na majimbo ya uchaguzi, baada ya uboreshaji wa daftari la kudumu la
wapigakura na muda mfupi uliotolewa kujiandikisha na uwekaji wazi wa daftari la
awali la wapiga kura.
Alisema
tathimini inaonesha katika baadhi ya maeneo, watu waliojitokeza kupiga kura ni
wachache, ukilinganisha na idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye daftari
la kudumu la wapiga kura.
“Baadhi
ya sababu zilizotolewa ni pamoja na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa kupiga kura
kutokana na elimu ya mpigakura kutowafikia wapigakura wengi, pia wapigakura
walijiandikisha katika daftari la kudumu kwa ajili ya matumizi mengine ili
kupata kadi kwa ajili ya matumizi mengine na uwepo wa hofu, vitisho na vurugu
siku ya kupigakura,” alisema.
Waziri
Mhagama, Mkurugenzi wanena
Kwa
upande wake, Waziri Mhagama alisema tume inapaswa kupongezwa kwa kukamilisha
zoezi zima la Uchaguzi Mkuu, ambalo lilikuwa na changamoto nyingi na ushindani
mkubwa wa kisiasa.
Alisema
kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura 343, tume
inapaswa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili kati ya Uchaguzi
Mkuu mmoja na mwingine, lakini haikuwezekana kufanyika hivyo baina ya mwaka
2010 na mwaka 2015 kutokana na sababu mbalimbali.
Alisema
sababu hizo ni pamoja na ufinyu wa bajeti na kuchelewa kupatikana kwa fedha kwa
wakati, lakini serikali itajitahidi kuhakikisha kuwa mapungufu yaliyo ndani ya
uwezo wake, yanatatuliwa ili kuiwezesha tume kutekeleza majukumu yake ya
kikatiba na kisheria kwa wakati.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima alisema tathimini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015
ilifanyika, ikiwa ni hatua ya kukamilisha mzunguko wa uchaguzi.
Alisema
kati ya watendaji 1,029 waliohojiwa, watendaji 929 ambao ni sawa na asilimia
90.3 walisema wana uelewa kuhusu muundo wa tume na watendaji 100 sawa na
asilimia 9.7, walikuwa hawana uelewa kuhusu muundo wa tume.
“Kati
ya watendaji 929 wa uchaguzi waliohojiwa, 818 sawa na asilimia 88 walisema kuwa
muundo wa tume unafaa kuendesha uchaguzi, aidha watendaji 111 sawa na asilimia
12 walieleza kuwa muundo wa tume haufai katika kuendesha uchaguzi,” alisema.
Pia
matokeo yanaonesha kuwa, katika watendaji wa uchaguzi 1,014 waliohojiwa, 814
sawa na asilimia 80.3 walisema hakukuwa na changamoto katika njia hizo,
watendaji 200 sawa na asilimia 19.7 walieleza njia za mawasiliano zilikuwa na
changamoto.
Alisema
matokeo ya tathimini yameonesha kati ya watendaji 1,029 waliohojiwa 996 sawa na
asilimia 96.8 walikuwa na maoni kuwa utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi
ulizingatia maelekezo yaliyotolewa na tume, ambapo watendaji 33 sawa na
asilimia 3.2 walieleza kuwa utekelezaji haukuzingatia maelekezo hayo.
Aidha
alisema wadau wa uchaguzi 1,915 waliohojiwa kuhusu uelewa wao juu ya elimu ya
mpiga kura, kati ya wadau 1,463 sawa na asilimia 76.4 walisema walikuwa na
uelewa wa elimu ya mpiga kura na 452 sawa na asilimia 23.6 hawakuwa na uelewa.
Kailima
alisema wapiga kura 499 walihojiwa, ambapo kati yao wapiga kura 377 sawa na
asilimia 75.6 walisema walitumia chini ya dakika 30 kufika kituo cha kupiga
kura, wakati wapiga kura 87 sawa na asilimia 17.5 walitumia dakika 30 hadi 60
kufika kituo cha kupiga kura.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ JAJI LUBUVA ATAKA TUMEYA UCHAGUZI IFUMULIWE..APENDEKEZAWAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAWEKWE KANDO KWENYE USIMAMIZI”
Post a Comment