Friday, October 28, 2016
MATOKEO YA DARASA LA SABA:MAJINA YA WATAHINIWA10 WALIOFANYA VIZURI NA SHULE 10 BORA.
Do you like this story?
Ufaulu kwa
watahiniwa wa mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2016 umepanda kwa asilimia
2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana
waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.
Matokeo hayo
yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA),
Dk Charles Msonde ambaye alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri
katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya
Tusiime ya jijini Dar es Salaam.
Kati ya
wanafunzi hao 10, watahiniwa saba wanatoka Shule ya Msingi Kwema iliyopo mkoani
Shinyanga, wawili Tusiime na mmoja kutoka Kaizirege ya Bukoba mkoani Kagera. Dk
Msonde alisema jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani
huo wamefaulu kwa kupata jumla ya alama 100 na zaidi kati ya alama 250.
“Idadi hii
ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni
283,751 na wavulana 271,540. Mwaka 2015 ufaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwapo
ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52,” alisema Dk Msonde.
Watahiniwa
16,929 wamepata daraja A, watahiniwa 141,616 wamepata Daraja B, watahiniwa
396,746 wamepata daraja C, watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872
wakipata daraja E . Dk Msonde alisema ufaulu katika masomo ya Sayansi na
Maarifa ya Jamii umepanda kwa asilimia kati ya 4.06 na 14.76 ikilinganishwa na
mwaka 2015 huku masomo ya Kiswahili, Hisabati na Kiingereza ufaulu umeshuka kwa
asilimia kati ya 0.39 na 12.51 ukilinganisha na mwaka jana.
“Watahiniwa
wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu wake ni asilimia 76.81
na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini ni Kiingereza lenye ufaulu wa
asilimia 36.05,” alifafanua Dk Msonde.
Dk Msonde
aliwataja watahiniwa waliofanya vizuri na shule zao kwenye mabano kuwa ni
Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema), Justina na Shabani
Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin
Benevenuto (Kwema) na Azad Ayatullah (Kaizirege).
Wasichana 10
bora ni Justina na Danielle Onditi (Tusiime), Linda Mtapima (Kaizirege), Cecilia
Kenene (Mugini), Magdalena Deogratias (Rocken Hill), Asnath Lemanya (Tusiime),
Fatuma Singili (Rocken Hill), Ashura Makoba (Kaizirege), Rachel Ntitu (Fountain
of Joy) na Irene Mwijage (Atlas).
Wanafunzi
wavulana 10 bora kitaifa, Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala
(Kwema), Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu
na Benjamin Benevenuto (Kwema), Azad Ayatullah (Kaizirege) na Benezeth Hango
(Kwema).
Shule 10
bora ni Kwema na Rocken Hill (Shinyanga), Mugini (Mwanza), Fountain of Joy na
Tusiime (Dar es Salaam), Mudio Islamic (Kilimanjaro), Atlas (Dar), St Achileus
(Kagera), Giftskillfull (Dar) na Carmel (Morogoro).
Shule 10
ambazo hazikufanya vizuri ni Mgata, Kitengu, Lumba Chini (Morogoro), Zege na
Kikole (Tanga), Magunga ya Morogoro, Nchinila ya Manyara, Mwabalebi (Simiyu)
Ilorienito (Arusha) na Chohero ya Morogoro.
Mikoa 10
iliyoongoza kitaifa ni Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza,
Kilimanjaro, Arusha, Njombe na Tabora wakati Halmashauri 10 bora ni Mpanda
Manispaa, Geita Mji, Arusha Mji, Mafinga Mji, Chato, Mwanza Jiji, Moshi Mji,
Mji Makambako, Ilemela na Hai.
Dk Msonde
alizitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri ni Mgata (Morogoro), Kitengu
(Morogoro), Lumba Chini (Morogoro), Zege (Tanga), Kilole (Tanga), Magunga
(Morogoro), Nchinila (Manyara), Mwabalebi (Simiyu), Ilorienito (Arusha) na
Chohero (Morogoro).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MATOKEO YA DARASA LA SABA:MAJINA YA WATAHINIWA10 WALIOFANYA VIZURI NA SHULE 10 BORA.”
Post a Comment