Friday, October 28, 2016
RIPOTI YA MKATABA WA LUGUMI..POLISI YAFIKA KWA SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI
Do you like this story?
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi, Projestus Rwegasira amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa
maagizo ya Bunge ya kuhakikisha mfumo wa vifaa vya utambuzi wa alama za vidole
unafungwa katika wilaya za kipolisi 108 nchi nzima kwa muda wa miezi mitatu.
Zabuni ya kufunga na kusambaza
mashine hizo za utambuzi wa vidole katika Jeshi la Polisi ulifanywa na Kampuni
ya Lugumi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati
hiyo Naghenjwa Kaboyoka, aliwathibitishia waandishi wa habari mjini Dodoma jana
kuwa ripoti hiyo tayari imekabidhiwa kwa Ofisi ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Kaboyoka alisema ripoti hiyo baada ya
kukabidhiwa kwa Spika Ndugai ataipitia na baadaye kuiwasilisha kwa kamati hiyo
ya PAC.
Juni 30, mwaka huu, Naibu Spika wa
Bunge, Dk Tulia Ackson baada ya kuahirisha Bunge la Bajeti aliiagiza serikali
kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ajili ya kuwadhibiti wahalifu na kuitaka
Kamati ya PAC ifuatilie suala hilo.
Dk Tulia alitoa agizo hilo baada ya
kupokea taarifa yenye utata ya kuhusu zabuni yenye thamani ya Sh bilioni 37 ya
kufunga mashine hizo katika vituo vyote vya Polisi baina ya Jeshi la Polisi na
Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited iliyotolewa mwaka 2011.
“Ninashauri serikali
ihakikishe mradi huu unakamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia
leo…, mradi huu utasaidia Jeshi la Polisi kuwatambua kwa haraka watu
waliohusika katika matukio ya uhalifu mbalimbali,” alisema.
Katika mkataba huo, Lugumi inatakiwa
kusambaza na kufunga mashine hizo za utambuzi wa vidole katika wilaya 108 za
kipolisi nchi nzima.
Hata hivyo, mashine hizo zilifungwa
kwenye vituo 14 pekee wakati tayari kampuni hiyo ilishapokea kiasi cha asilimia
99 za malipo yake.
Katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha 2013/14 ilionesha kuwa
pamoja na kampuni hiyo ya Lugumi kulipwa asilimia 99 ya malipo sawa na Sh
bilioni 34, bado haijakamilisha mradi huo kwa muda wa miaka mitano sasa.
Aprili, mwaka huu, PAC iliunda kamati
ndogo kwa ajili ya kuchunguza mkataba huo wa utata baina ya Kampuni ya Lugumi
na Jeshi la Polisi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RIPOTI YA MKATABA WA LUGUMI..POLISI YAFIKA KWA SPIKA WA BUNGE, JOB NDUGAI”
Post a Comment