Friday, October 28, 2016
SUMAYE KUNYANG"ANYWA SHAMBA NA SERIKALI, APEWA SIKU 90
Do you like this story?
Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema hati ya shamba lililopo maeneo ya
Bunju la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fredrick
Sumaye liko katika hatua ya kufutwa na kwamba Afisa Ardhi Mteule wa Wilaya ya
Kinondoni Rehema Mwinuka ameshatoa barua ya notisi ya siku 90.
Lukuvi ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam
wakati akizungumza na wandishi wa habari.
“Shamba la Sumaye hati
yake iko katika hatua za kufutiwa,
Afisa Ardhi Mteule wa
Wilaya ambaye anajukumu la kutoa notisi, ameshatoa notisi kwamba hajaendeleza
eneo hilo kwa muda mrefu hivyo kwa mujibu wa sheria hati yake inatakiwa
kufutwa,” alisema.
Alisema serikali haitofumbia macho
wamiliki wa ardhi na mashamba ambao hawajayaendeleza kwa muda mrefu.
Pia, kufuatia ongezeko la matapeli
wanaotumia nyaraka za kughushi za barua za toleo (ofa) zinazodaiwa kutolewa na
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Lukuvi alitoa agizo hususani kwa wakazi
wa jiji hilo wanaomiliki ardhi pasipo kuwa na hati miliki, kujisalimisha kwa
kupeleka barua zao za ofa kwa Kamishna wa Ardhi ili wapatiwe hati halali.
“Wamiliki wote
wanaomiliki ardhi kwa karatasi za ofa halali wazibadilishie ili wapewe hati
halali, na atakaegundulika kumiliki ofa feki polisi watawakamata na kupelekwa
mahakamani,” alisema.
Alisema asilimia 60 ya watu
wanaopeleka kesi za migogoro ya ardhi wizarani, chanzo cha migogoro hiyo ni
karatasi za ofa zinazotoka katika halamshauri za jiji na manispaa.
“Natoa miezi mitatu ili
karatasi hizi zisitokee tena kila mtu alete barua ya ofa watapewa hati zao
ndani ya mwezi mmoja ,wazilete kwa kamishna wa ardhi wa mkoa, baada ya hapo
sitasikiliza malalamiko ya watu walioibiwa ardhi wakiwa na ofa ya namna hii.
“Tumieni miezi mitatu
vizuri kubadilisha ofa,” amesema.
Hali kadhalika, Lukuvi alipiga
marufuku vitendo vya uvamizi wa ardhi na mashamba vinavyofanywa na baadhi ya
wananchi, na kuwataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini kuwa kuna
shamba au ardhi isiyoendelezwa.
“Serikali ina laani
uvamizi wa ardhi na mashamba unaofanywa na baadhi ya wananchi sababu baadhi yao
yanamilikiwa kihalali na yana hati, serikali ipo na sheria zipo zitafanya kazi
yake,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SUMAYE KUNYANG"ANYWA SHAMBA NA SERIKALI, APEWA SIKU 90”
Post a Comment