Sunday, October 30, 2016
TAMBWE AMKIMBIZA KICHUYA KIMYA KIMYA YANGA WAKIITANDIKA MBAO UHURU
Do you like this story?
Yanga
SC leo ni kama wamewajibu wapinzani wao Simba baada ya kuibuka na ushindi mnono
wa mabao 3-0 dhidi ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza, mchezo uliofanyika Uwanja
wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kipindi
cha kwanza kilianza kwa kila upande kuwa mgumu huku wakicheza kwa kuviziana,
hali iliyopelekea mchezo kuwa mgumu kwa pande zote.
Yanga
ambao leo kwa mara ya kwanza walikuwa chini ya kocha Hans Van der Pluijm
aliyerudi baada ya kubatilisha maamuzi yake ya kujiuzulu, safu yao ya
ushambuliaji ilianza chini ya Amissi Tambwe na Obrey Chirwa.
Mpaka
kipindi cha kwanza kinamalizika, milango ya timu zote ilikuwa migumu baada ya
timu zote kutoshana nguvu.
Kipindi
cha pili Yanga waliingia kwa kasi kubwa wakitafuta bao la mapema ili kujiweka
katika mazingira mazuri, hasa baada ya watani wao Simba kushinda kwa kishindo
jana dhidi ya Mwadui FC mjini Shinyanga.
Dakika
ya 50 Yanga walipata bao la kwanza kupitia kwa beki wake Mtogo Vincent Bossou
baada ya kuunganisha mpira mzuri wa adhabu ndogo uliopigwa na Haruna Niyonzima
aliyekuwa nahodha katika mchezo wa leo.
Yanga
waliendelea kulisakama lango la Mbao FC na kufanikiwa kupata bao la pili dakika
ya 57 baada ya makosa ya kipa wa Mbao Emmanuel Mseja kushindwa kuudaka mpira
uliorushwa na Mbuyu Twite.
Dakika
ya 65 Yanga walifanya mabadiliko kwa beki wao wa kulia Hassan kessy kwenda
benchi na Thabani Kamusoko kuchukua nafasi hiyo.
Amissi
Tambwe ambaye kwenye mchezo wa leo alifichwa kwa muda fulani wa mchezo, aliifungia
Yanga bao la tatu baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Simon Msuva dakika ya
76.
Kipa
wa Yanga Deogratius Munishi alipewa kadi ya njano dakika ya 88 baada ya
kuchelewesha muda kwa makusudi.
Matokeo
ya leo yanaibakisha Yanga katika nafasi ya pili wakiwa na alama 27 nyuma ya
vinara mahasimu wao Simba wenye alama 32.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAMBWE AMKIMBIZA KICHUYA KIMYA KIMYA YANGA WAKIITANDIKA MBAO UHURU”
Post a Comment