Saturday, October 29, 2016
UFISADI NSSF: CCM YATAKA AKAUNTI ZA ZITTO KABWE ZIPEKULIWE
Do you like this story?
Serikali imefanikiwa kurejesha udhibiti wake kwenye Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) baada ya kurejeshewa asilimia 52 ya hisa zilizonunuliwa kinyume na utaratibu na Kampuni ya Simon Group Limited (SGL).
Kurejeshwa
kwa hisa hizo kunatokana na ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), kwamba mauzo ya hisa hizo yaliyofanywa na Bodi ya Wakurugenzi
wa Uda hayakuwa na kibali cha Serikali.
Ripoti
ya CAG ya mwaka 2014/15 ilibainisha licha ya utaratibu kukiukwa pia hakuna vilelezo
vya fedha za manunuzi zaidi ya kuonyesha Sh320 milioni ziliingizwa kwenye
akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa Bodi, Idd Simba ambazo hata hivyo alidai ni
malipo ya ushauri alioutoa kwa mwekezaji huo.
Kurejeshwa
kwa hisa hizo, kutolewa taarifa ndani ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
za Mitaa (LAAC) ambayo Jumanne ya wiki hii iliuweka kikaangoni uongozi wa Jiji
la Dar es Salaam kuhusiana na sakata la Uda.
Pia,
kamati iliwataka Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi) George Simbachawene, Mwanasheria Mkuu wa Serikali
George Masaju na Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru wafike kwenye kamati wakiwa
na majibu sahihi kuhusu sakata hilo.
Viongozi
hao waliitikia wito huo jana, na baada ya kikao cha faragha Mwenyekiti wa LAAC
, Vedasto Mwiru alisema Serikali imeitaarifu kamati yake kuwa imerejesha katika
himaya yake fungu kuu la hisa ambazo hazikugawiwa.
Mwiru
alisema Serikali imerejesha hisa asilimia 52 ambazo ziliuzwa na Bodi ya
Wakurugenzi Wa Uda kinyume cha utaratibu.
“Maelezo
yaliyotolewa na Serikali zile share (hisa) zote ambazo hazikugawiwa ziko
salama chini ya mikono salama ya Serikali hazijauzwa,” alisema.
Mwiru
ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), alisema kutokana na maelezo hayo
wabunge wametaka mikataba ya kurudisha hisa hizo kwa Serikali ipelekwe kwenye
kamati hiyo.
Alisema
kamati hiyo inaipa Serikali muda wa wiki mbili kuhakikisha kuwa wanawasilisha
nyaraka hizo.
Meya
wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita alisema wanasubiri majibu ya barua yao ya
kuomba ushauri kuhusu uuzwaji wa hisa za jiji za asilimia 51 kutoka kwa
mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Alisema
baada ya kupokea ushauri huo watapeleka katika Baraza la Madiwani ili kuona
namna ya kwenda mbele pamoja na kuzifanyia kazi fedha walizouza hisa zao ambazo
ziko katika Benki Kuu (BoT).
Mwanasheria
Mkuu Masaju alisema anakwenda kuandika mambo yote yaliyosemwa ili iwasaidie
kamati na Jiji la Dar es Salaam kukamilisha utaratibu huo kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ UFISADI NSSF: CCM YATAKA AKAUNTI ZA ZITTO KABWE ZIPEKULIWE”
Post a Comment