Friday, October 28, 2016

WATUNGUAJI WAWILI WA HELIKOPTA PORI LA AKIBA, SIMIYU WAHUKUMIWA KWENDA JELA.


SIMIYU: Mahakama ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu imewahukumu kwenda jela miaka kumi watuhumiwa wawili ambao ni miongoni mwa watuhumiwa kumi waliokuwa wakituhumiwa na kesi ya kutungua helikopta ya kampuni ya Mwiba Holings katika pori la Akiba la Maswa Maswa lililoko Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti mwezi January mwaka huu. 

Katika tukio hilo aliyekuwa rubani wa helkopita hiyo Roger Gower raia wa Uingereza aliuawa sambamba na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.

Waliokumbwa na hukumu hiyo ni Doto Huja Kubeja na Mwigulu Kanga wote wakazi wa wilaya ya Meatu ambapo katika kesi hiyo walikuwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya kumiliki silaha na kumiliki risasai kinyume cha sheria.

Awali imedaiwa mahakamani hapo na wakili kiongozi wa serikali Grace Mpatili mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhizi wa Mahakama ya wilaya hiyo,Mary Mrio kuwa mnamo January 23,mwaka huu na February 2 mwaka huu huko wilayani Meatu washitakiwa walikamatwa na askari polisi wakiwa na bunduki moja aina ya Raifo pamoja na risasi kinyume cha sheria.


Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mrio amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamahuri pasipo kuacha shaka na hivyo mahakama imewakutana hatua na hivyo imewahukumu kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa kila mmoja ili liwe fundisho kwa watu wengine.

0 Responses to “WATUNGUAJI WAWILI WA HELIKOPTA PORI LA AKIBA, SIMIYU WAHUKUMIWA KWENDA JELA.”

Post a Comment

More to Read