Friday, October 28, 2016

WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA JANE GOODALL INSTITUTE


Shirika lisilo la Kiserikali la Jane Goodall linalojishughulisha na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori wengine limepongezwa kwa jitihada zake za kutunza mazingira na kusaidia jamii kuhifadhi mfumo wa ikolojia ukanda wa Magharibi mwa Tanzania.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba mara baada ya kutembele Ofisi zao Mkoani Kigoma. Waziri Makamba amesema kuwa Shirikal hilo la Jane Goodall limekuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi ambayo inagusa jamii moja kwa moja.

Akitoa maelezo ya shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo kwasasa, Naibu Mkurugenzi wa Bi. Mary Mavanza amesema kuwa wanatekeleza miradi mitatu ikiwa ni pamoja na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori, Mradi wa Mizizi na chipukizi ambao unatekelezwa nchi nzima katika shule zote na mradi wa uhifadhi unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Mpanda, Nsimbo kwa Mkoa wa Katavi na Uvinza kwa Mkoa wa Kigoma.

Aidha, Shirika hili pia limefanikiwa kuhamasisha wanajamii 42 kufanya shughuli za kukuza kipato ambazo ni rafiki kwa mazingira kupitia ufugaji nyuki na huduma za kiikolojia. Pamoja na mafanikio hayo shirikali hili limewasilisha hoja ya kwa Waziri Makamba kusaidia kukamilika kwa Mchakato wa kupandisha hadhi ya ardhi jumla kuwa misitu ya Hifadhi ya Wilaya ili kudhibiti idadi kubwa ya sokwe waliobaki Tanzania ambao kwa sasa hawana ulinzi thabiti.

Taasisi ya Jane Goodall liliasisiwa miaka 56 iliyopita na mtafifiti Dr. Jane Goodall kwa lengo la kufanya shughuli za kitafiti, kurejesha uoto wa asili uliopotea na kuhakikisha wanajamii wanaboresha uchumi wao kwa kutumia maliasili zinazowazunguka.

Waziri Makamba pia ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa lengo la kufuatilia changamoto za kimazingira Hifadhini hapo.
Na Lulu Mussa, Kigoma


0 Responses to “WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA JANE GOODALL INSTITUTE”

Post a Comment

More to Read