Sunday, October 30, 2016

RAIS WA TANZANIA DK JOHN POMBE MAGUFULI ANATARAJIA KUANZA ZIARA YAKE HAPO KESHO NCHINI KENYA




Kwa mara ya kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, atazuru taifa jirani la Kenya hapo kesho Jumatatu.

Ziara ya Magufuli nchini humo, inatukia wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegea.
Kwenye ajenda ya ziara hiyo rasmi ya kiserikali, kati yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili, kwani Rais magufuli amekosa kuhudhuria mikitano mikuu miwili jijini Nairobi, iliyowaleta pamoja marais wengi wa Afrika.

Tangu aingie mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli ambaye ameamua kukabiliana na ufisadi nchini mwake amezuru tu Rwanda na Uganda.

Pia ziara ya Dkt Magufuli inahusia na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa muungano wa afrika-AU.

Tofauti na Tanzania, kashfa za mamilioni ya dola inafichuliwa mara kwa mara nchini Kenya, huku pesa za umma zikinyakuliwa na baadhi ya watu mashuhuri serikalini na walio na uhusiano wa karibu na watawala wa nchi hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta atamkaribisha mgeni wake jijini Nairobi, baada ya Kenyatta kukamilisha ziara ya siku mbili huko Khartoum, alipokutana na Rais wa Sudan- Omar Al- Bashir.

0 Responses to “ RAIS WA TANZANIA DK JOHN POMBE MAGUFULI ANATARAJIA KUANZA ZIARA YAKE HAPO KESHO NCHINI KENYA”

Post a Comment

More to Read