Friday, March 7, 2014

KOCHA DAVID MOYES AANDIKA BARUA KWENDA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED.


Kocha wa Manchester United David Moyes.


Kocha wa Manchester United David Moyes ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa klabu hiyo akielezea kwamba msimu wake wa kwanza ndani ya klabu umekuwa m'bovu zaidi kuliko ilivyotegemewa.

Akiwasifu mashabiki kwa uvumilivu wao, Mscotish ambaye aliteuliwa na Sir Alex Ferguson, amekiri kwamba matokeo yao mabovu yamemshangaza mpaka yeye lakini ana uhakika kila kitu kitakaa sawa mbeleni.

"Wakati nilifahamu hii kazi ingekuwa na changamoto nyingi wakati nilipopewa jukumu hili, lakini msimu mgumu tulionao hakikuwa kitu ambacho nilikifiria, jambo ambalo nina uhakika mashabiki wote hawakudhani hali ingekuwa hivi," aliandika Moyes.
 
"Wachezaji wangu, na makocha wenzangu wanajaribu kwa kila kuhakikisha timu inarudi katika kufanya vizuri.
"Wote tumezoea kuiona Manchester United inayofanikiwa na sapoti mliyowapa wachezaji na mimi katika kipindi chote cha msimu ni kubwa sana.

 Tunapocheza ugenini mashabiki wetu waliosafiri wameendelea kuwa bora kabisa katika nchi hii na wakati tunapokuwa Old Trafford imani yenu kwenye timu imekuwa ikionekana wazi.

0 Responses to “KOCHA DAVID MOYES AANDIKA BARUA KWENDA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED.”

Post a Comment

More to Read