Thursday, March 20, 2014
TRA MBEYA YAKIRI WINGI WA KODI NCHINI.
Do you like this story?
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa
Mbeya imekiri kuwepo kwa utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara ambazo sasa ni
kero kwao na kwamba sasa inaangalia upya njia sahihi ya kuzikusanya kwa
pamoja.
Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA wa Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini, Kissa Kyejo alitoa kauli hiyo mjini Chunya juzi,
wakati akijibu kero mbalimbali za wafanyabiashara, kwenye semina
iliyoandalia na TRA.
Semina hiyo ilihusu umuhimu kwa mfanyabiashara
kulipa kodi kwa kutumia Mfumo wa Mashine za Ki-eletroniki (EFDs).
Kissa amesema wafanyabiashara maeneo mengi
wamelalamikia kuwapo kwa utitiri huo na kwamba hata TRA wameliona, na
sasa walishapeleka ombi kwao ili ziweze kuunganishwa kwa pamoja.
Awali wafanyabiashara hao walilalamikia
kuwapo aina mbalimbali za kodi ambazo walidai zimekuwa
kero kubwa kwao, ikiwamo usumbufu wanaoupata kutoka kwa maafisa wa
Serikali.
Mfanyabiashara wa Chunya Mjini, Ayubu Omari amesema:
“Leo anakuja mtu wa TRA, tunamalizana naye, kesho mtu wa ardhi, mara wa
maji, hujakaa sawa watu wa halmashauri nao wamefika wanataka ushuru. Sasa
huu utitiri wa kodi kwetu tunaona ni usumbufu na kero.’
’
Akifungua semina hiyo, Mkuu wa Wilaya ya
Chunya, Deodatus Kinawiro aliwataka wafanyabiashara hasa wachimbaji wadogo
wa dhahabu kupitia Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Mbeya,
(Mberema) kuanza kulipa kodi. Amesema wachimbaji wengi wanapata
fedha nyingi, lakini hawalipi kodi na hivyo kuikosesha serikali mapato.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TRA MBEYA YAKIRI WINGI WA KODI NCHINI.”
Post a Comment