Saturday, March 8, 2014

WAZIRI SOPHIA SIMBA APATA MSIBA MZITO, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AENDA KUMFARIJI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwa Waziri Masaki jijini Dar es Salaam, kutoa pole.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, wakati alipofika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, kutoa pole kwa kufiwa na mtoto wake, Lefoord Simba. Mazishi yatafanyika leo kwenye Makaburi ya Kinondoni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa, Waziri mstaafu (wa pili kulia) Mjumbe wa Nec Wilaya ya Busega, Chegeni (kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, wakizungumza jambo wakati wakijumuika kwa pamoja katika maombolezo ya msiba wa Lefoord Simba, mtoto wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, Masaki jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waombolezaji. (picha: Ofisi ya Makamu wa Rais)

0 Responses to “WAZIRI SOPHIA SIMBA APATA MSIBA MZITO, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AENDA KUMFARIJI”

Post a Comment

More to Read