Wednesday, April 16, 2014
FERRY YAZAMA KOREA.
Do you like this story?
Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini. |
Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura
zilizoripotiwa kutoka meli moja ilioyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya
Korea Kusini.
Maafisa
wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege
za uokoaji , zimepelekwa katika ferry moja inayozama kusini mwa pwani hiyo.
Shughuli
zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Jeshi
la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi
ya Korea.
Maafisa
wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi
kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju
.
Waokoaji
wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke
baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia
wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kusakama maji
zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.
Shughuli
ya uokoaji bado inaendelea huku duru zikidhibitisha kuwa mtu mmoja amepatikana
ameaga dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FERRY YAZAMA KOREA.”
Post a Comment