Saturday, April 19, 2014
HIVI NDIVYO MELI ILIVYOZAMA ZIWA VICTORIA.
Do you like this story?
Watu 10 wamenusurika kufa maji katika ziwa Victoria baada ya meli ya
mizigo Fb Matara kupinduka na kuzama ikiwa na shehena ya sukari tani 280
zilizonunuliwa katika kiwanda cha sukari Kagera wakati ikitoka Bukoba kwenda
jijini Mwanza.
Meli hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Mkombozi fishing and marine
transport limited, imezama ikiwa na magunia 5600 ya sukari sawa na tani 280,
mali ya mfanyabiashara wa jijini Mwanza aitwaye V.h. Shah, ambapo mkurugenzi wa
kampuni hiyo Gitano Chacha Munanka ameeleza kwamba meli hiyo imezama ikiwa
katikati ya visiwa vya Kerebe na Lukolu majira ya saa 10.30 usiku na kuongeza
kwamba hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kufuatia tukio hilo.
ITV imeshuhudia meli hiyo ikiwa imepinduka huku juhudi za wafanyakazi wa
kampuni hiyo kuipundua zikiwa zinaendelea bila mafanikio, huku baadhi ya
mashuhuda wa tukio hilo wakisema chanzo cha meli hiyo kuzama ni kutokana na
dhoruba kali ambapo wametoa ushauri kwa wamiliki wa vyombo vya majini
kuzingatia utabiri unaotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kuepusha
maafa.
Meli hii inayoonekana pichani ni mfano wa meli iliyozama,ambayo ilianza
safari yake ya kutoka Bukoba majira ya saa 7 mchana, ikiwa inaendeshwa na
kapteni Erick Lasana – mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu
Sumatra kanda ya ziwa, umethibitisha kuzama kwa meli hiyo yenye uwezo wa kubeba
tani 280 za mizigo na abiria 100.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HIVI NDIVYO MELI ILIVYOZAMA ZIWA VICTORIA.”
Post a Comment