Thursday, April 10, 2014
KAMATAKAMATA YA PIKIPIKI NA BAJAJ YASHIKA KASI JIJINI DAR, JIONEE MWENYEWE HALI ILIVYOKUWA.
Do you like this story?
Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi. |
Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa |
Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa. |
Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi. |
Oparesheni
Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake kutoka Mwenge na
maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa
Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge
kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar
limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.
Kwa mujibu wa
Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake
alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na
bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu
sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana
wameamua kuzuia.
“Tumefanya hivi
ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana
unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza
tatizo hili.
Tulicho
kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge
kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala
ndogo”Hiace” pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji
elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa”
alimalizia kwa kusema “Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale
ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali”
alisema Polisi huyo.
Kwa mujibu wa
madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao
wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali
iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo.
Wanao
ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi
na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAMATAKAMATA YA PIKIPIKI NA BAJAJ YASHIKA KASI JIJINI DAR, JIONEE MWENYEWE HALI ILIVYOKUWA.”
Post a Comment