Thursday, April 10, 2014

VIROBA VYA KONYAGI FEKI WAPANDISHWA MAHAKAMANI MOSHI.






MAHAKAMA ya hakimu mkazi Moshi, leo imefurika mamia ya wananchi waliokwenda kushuhudia watuhumiwa sugu wa utengenezaji wa konyagi feki na bidhaa nyingine mbalimbali na kuzibandika nembo za TRA ambayo inadiwa kudhuru maelfu ya watanzania.

Hata hivyo mahakama ya mkazi moshi imetoa kwa dhamana watuhumiwa hao nane ambao wanakabiliwa na tuhuma za kutumia alama za biashara za makampuni mengine kwa nia ya kutapeli.na kujipatia pesa kinyume cha utaratibu.

Watuhumiwa hao ni Yusuph George, Richard Leonard, Preygod Urassa, Mohamed Rashid, Greyson Jonathan, George Kisivani, Hagai Nelson na Jackson Shayo, ambao wanatuhumiwa kwa pamoja kwa
kutumia kwa nia ya kutapeli alama ya biashara ya Konyagi kinyume cha sheria huku wakijua wazi ya kuwa alama hiyo ni ya kibiashara ya halali ya kampuni ya Tanzania Distilleries Limited.

Watuhumiwa hawa wana kesi mbalimbali ikiwemo ile ya kutumia nyaraka za mamlaka ya mapato nchini TRA ikiwemo mihuri yenye namba za kodi ya mapato jambo ambalo linadaiwa kuikosesha serikali mapato mengi.

Wakili wa serikali Julius Semali ameiambia mahakama ya mkazi Moshi kuwa watuhumiwa hao ni hatari na kwamba wanakabiliwa na kesi za namna hiyo maeneo mbalimbali hapa nchini.

Singida wana kesi ya namna hii na ambayo itaendelea tena Aprili   30, 2014, Ilala wanatafutwa na polisi kwa kukutwa na nyaraka za TRA wakati Arusha wanatafutwa kwa kukiuka dhamana na kutoroka mwaka 2012.

Pamoja na kupewa dhamana kwenye kesi hiyo huko Moshi, bado hakimu aliamuru warudishwe rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Kesi hii imevutia mamia ya wakazi ambapo miongoni mwao ambao ni wafanyabiashara za mabaa wametoa wito kwa wananchi kuepuka kunywa konyagi vichochoroni kutokana na madhara ambayo wameshapata watu wengi.

0 Responses to “VIROBA VYA KONYAGI FEKI WAPANDISHWA MAHAKAMANI MOSHI.”

Post a Comment

More to Read