Thursday, June 19, 2014
POLISI YAPIGA MARUFUKU NGOMA ZA BUNYEROBUNYERO
Do you like this story?
Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam imesema itawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa
klabu za usiku zinazokiuka maadili kwa kuruhusu klabu zao kupiga ngoma ya
‘bunyerobunyero’.
Ngoma hiyo
iliibuka na kuwa maarufu hasa jijini Dar es Salaam baada ya Polisi kupiga
marufuku ngoma ya ‘kantangaze-kigodoro’ na ‘khanga moko’.
Onyo hilo
lilitolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kanda hiyo, Suleiman Kova wakati
akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ngoma
hiyo imeibuka karibuni na inaenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
Alisema ngoma
hizo hazina tofauti kubwa na vigodoro isipokuwa wahusika wa ‘bunyerobunyero
wametofautisha maeneo ya kupinga ngoma hiyo ambayo ni kwenye klabu za usiku
tofauti na vigodoro ilikuwa ikipigwa mitaani.
“Tutahakikisha
kwa kushirikiana na halmashauri za miji pamoja na polisi kuhakikisha hizi ngoma
za ‘bunyerobunyero’ tunazipiga marufuku, kwasababu zinakiuka maadili,” alisema
Kova.
Alisema
Polisi imetoa onyo mara nyingi kuhusu ngoma hizo na kwamba hatua inayofuata
sasa ni kuwakamata wachezaji na wahudhuriaji wa ngoma hizo pamoja na kuwakamata
wamiliki wa klabu hizo na kuwapiga faini na kuzifungia klabu hizo.
“Onyo hili
linatolewa kwasababu hizi ngoma zimeenea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la
Dar es Salaam,” alisema.
Kamanda Kova
alisema ngoma hizo zimetawaliwa na udhalilishaji wa hali ya juu jambo
linalochangia kuporomoka kwa maadili, hivyo hawatalifumbia macho.
“Uchunguzi
kwasasa unafanyika na endapo itabainika ngoma hizo kuendelea kuchezwa basi
Jeshi la Polisi na halmashauri za miji zitachukua hatua mbalimbali za kisheria
ikiwa ni pamoja na kuzifungia klabu hizo kwasababu zinakiuka taratibu za
leseni,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI YAPIGA MARUFUKU NGOMA ZA BUNYEROBUNYERO ”
Post a Comment