Tuesday, July 8, 2014

BOMU LALIPUKA ARUSHA KATIKA MGAHAWA WA TRADITIONAL INDIAN CUSINE NANE WAJERULIWA


 mmoja wa mtu alielipuliwa na bomu katika mgahawa wa
Traditional Indian Cusine aliyejukilana kwa jina la Deepak Gupta (25)
akiwa amelazwa  katika hospitali ya seliani ndani ya  chumba cha
mahututi (ICU) mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto
kutokana na mguu huo kuumizwa sana na bomu hilo





Mlipuko unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha  katika mgahawa wa  Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane

Akithibitisha kupokea wagonjwa walioadhiriwa na bomu hilo  Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga  alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira yasaa 4:30 usiku katika eneo kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na saatano .

Alisema kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia upasuaji usiku huo huo.



“kati yawagonjwa hao nane mmoja alitwa akiwa mahututi sana kwani mguu wake ulikuwa umeadhiriwa sana na bomu hiloivyo ikatulazimu  kumkata mguu mmoja wa kushoto ,kwakweli mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak Gupta (25) mwanaume na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupokatika chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani”alisema Kisanga



Alisema kuwa  katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari



Aidha aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na  Vinod Suvesh(37), Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14) ,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25)  wote wakiwa na asili ya kiasia

Kisanga alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio  waliofika hapo hospitali walidai kuwa   bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.

0 Responses to “BOMU LALIPUKA ARUSHA KATIKA MGAHAWA WA TRADITIONAL INDIAN CUSINE NANE WAJERULIWA ”

Post a Comment

More to Read