Sunday, July 13, 2014
KAULI YA MWISHO YA BALALI KABLA YA KIFO CHAKE.
Do you like this story?
Dar na
Marekani. Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania BOT), Marehemu Daudi
Ballali aliacha wasia unaotaka maiti yake isionyeshwe hadharani atakapofariki
dunia na wala maiti yake isiletwe Tanzania kwa ajili ya maziko.
Ballali
aliyefariki Mei 16, 2008 na kuzikwa Mei 23 mwaka huohuo katika makaburi ya Gate
of Heaven, eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani alifahamu kuhusu
kifo chake wiki mbili kabla, baada ya matibabu kushindikana.
Mwandishi
wa Mwananchi aliyekuwa nchini Marekani kwa siku kumi kufuatilia suala hilo,
alibaini kuwa kiongozi huyo alilazwa mara ya pili katika Hospitali ya Chuo
Kikuu cha George Washington, April 2008 na alirejea nyumbani kwake, Washington
DC wiki mbili kabla ya kukutwa na mauti.
Habari
kutoka ndani ya familia yake zinasema baada ya madaktari kushindwa kumtibu
walimwambia kwamba asingeweza kuishi kwa zaidi ya wiki mbili, hivyo walimshauri
ahamie kwenye ‘hospice’ ambayo ni nyumba maalumu ya kusubiri kifo kwa watu
ambao magonjwa yao yameshindikana.
Hospice
hutumika kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa wanaohitaji faraja hasa kutoka na
maumivu makali chini ya uangalizi wa washauri na wauguzi kwa lengo la
kuwaongezea wagonjwa husika siku za kuishi.
Baadhi
ya hospice hutoa huduma za kiroho, kijamii na kifedha na wakati mwingine huduma
hizo hutolewa kwa wagonjwa ambao wanaugulia nyumbani. Hata hivyo, gazeti hili
lilidokezwa kwamba Ballali alikataa kwenda kwenye nyumba hiyo na badala yake
kutaka apelekwe nyumbani kwake.
“Alikataa
kwenda kwenye hospice, aliwaambia madaktari kwamba yeye hawezi kwenda huko
ijapokuwa kuna huduma nzuri na uangalizi wa nesi (muuguzi). Aliwaambia kwamba
nitakwenda kufia nyumbani kwangu maana nina nyumbani kwangu,” kilisema chanzo
chetu na kuongeza:
“Aliporejeshwa
nyumbani, alikuwa anazungumza kama kawaida lakini kadri siku zilivyosogea hali
ilikuwa ikibadilika na kama sikosei siku mbili au tatu za mwisho (za uhai wake)
alikuwa anajitambua lakini alikata kauli, hakuwa akizungumza chochote”.
Uchunguzi
wetu umebaini kuwa katika siku hizo za mwisho za uhai wake, Ballali aliacha
maelekezo kwamba pindi atakapofariki dunia, mwili wake usiwekwe hadharani kwa
maana ya kutazamwa na watu nje ya familia wala kusafirishwa kuja Tanzania kwa
ajili ya maziko.
“He
said, he doesn’t like to be turned into a laughing staff (alisema asingependa
kugeuzwa kichekesho), sababu watu wasingekuja kutoa heshima za mwisho, bali
wangekuja kumdhihaki kuangalia Ballali aliyetuhumiwa kwa ufisadi wa EPA na siyo
Gavana,” kilisema chanzo hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAULI YA MWISHO YA BALALI KABLA YA KIFO CHAKE.”
Post a Comment