Thursday, July 17, 2014

MABOMU ARUSHA, ZANZIBAR KUATHIRI MAPATO- MKUYA.



Waziri wa fedha saada salum mkuya  amesema matukio ya milipuko ya mabomu yanayotokea katika miji ya arusha na Zanzibar yanaleta madhara kiuchumu kwa vile yatapunguza idadi  ya watalii na uwekezaji.

Kutokana na hali hiyo makusanyo ya kodi na mapato mbalimbali ya serikali  nayo yatapungua  hivyo kuathiri kasi  ya ukuaji maendeleo.

Akizungumza mara baada ya kufungua kongamano  la majadiliano ya wadau wa kodi na mapato  kutoka nchi 19 ndani na nje ya afrika jijini arusha jana mkuya amesema arusha na Zanzibar ni mihimili ya mapato yanayotokana na sekta ya utalii na jambo lolote linaloathiri maeneo hayo huathiri  pia mapato kutoka sekta hiyo.

Arusha ni miongoni  mwa mikoa inayoongoza  kwa kukusanya  kodi nchini katika siku za karibuni makusanyo  yameshuka kuna sababu nyingi ikiwamo baadhi ya taasisi  za kimataifa mahakama ya kimataifa na mauji ya tranda kufunga  shughuli zao lakini pia milipuko ya mabomu imechangia kushuka mapato amesema mkuya.

Tofauti zinazojitokeza  miongoni  mwetu tusizimalize kwa kulipuana kwa mabumu kuna njia nyingi na bora za kutatua tofauti zetu ameseme mkuya.

Amesema  muda umefika kwa watanzania  kujitafakari  walipokosea hadi kufikia hatua ya kulipuana kwa mabomu.

Awali waziri mkuya aliwataka wataalamu wa kodi wawekezaji  na wasomi kutoka vyuo vikuu ndani na nje ya afrika wanaokutana jijini hapa kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto  za  ukusanyaji hafifu wa kodi  na mapato.

0 Responses to “MABOMU ARUSHA, ZANZIBAR KUATHIRI MAPATO- MKUYA.”

Post a Comment

More to Read