Wednesday, July 16, 2014
RAIS WA TFF AANDAA FUTARI KWA WADAU.
Do you like this story?
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ameandaa futari kesho (Julai 17 mwaka huu) kwa wadau mbalimbali
wa mpira wa miguu.
Shughuli hiyo itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam ambapo waalikwa wataanza kuwasili saa 11.30 jioni.
Waalikwa katika futari hiyo wametoka katika makundi
mbalimbali. Makundi hayo ni wadhamini, klabu za Ligi Kuu na Daraja la Kwanza za
Dar es Salaam ambazo zitawakilishwa na watu wawili wawili.
Viongozi wa zamani wa TFF, Said El Maamry, Leodegar
Tenga, Muhidin Ndolanga, Athuman Nyamlani, Mwina Kaduguda, Michael Wambura,
Fredrick Mwakalebela na Ashery Gasabile. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF waliopo
Dar es Salaam, Wizara ya Michezo na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Vyama shiriki; TWFA, TAFCA, TASMA, SPUTANZA, FRAT
ambavyo vitawakilishwa na watu watatu watatu, viongozi wa Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), wahariri
wa habari za michezo, Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
na Polisi kanda Maalumu- Dar es Salaam.
Wajumbe wa kamati ndogondogo za TFF waliopo Dar es
Salaam, wazee wa Simba na Yanga- watano kutoka kila klabu, timu ya Serengeti
Boys, klabu ya Saigon, Bodi ya Ligi Kuu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu
wa wilaya za Dar es Salaam, wabunge wa Dar es Salaam, Meya wa Dar es Salaam,
Meya wa Kinondoni, Meya wa Ilala na Meya wa Temeke.
Waalikwa wengine ni Omari Abdulkadir, Amin Bakhresa,
Harudiki Kabunju, Hamis Kissiwa, Ismail Aden Rage, Masoud Sanani, Jamal Bayser,
Hassan Dalali, Imani Madega na Mbaraka Igangula.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ RAIS WA TFF AANDAA FUTARI KWA WADAU.”
Post a Comment