Thursday, July 17, 2014

WANANCHI WAFANYIWA HUDUMA ZA KIAFYA CHINI YA MTI WILAYANI WANGING'OMBE MKOA WA NJOMBE.


 Akina mama wakutwa wakiendelea na Zoezi la Kuwapima watoto[kliniki]kwenye miti Huko Igenge kata ya Saja Mkoani Njombe


 Hili ni jengo la Soko lililojengwa na Serikali kupitia mradi wa TASSAF Lakini Halifanyi kazi yoyote na hivyo wananchi wataka kuligeuza Zahanati Kwa ajili ya Kupimia Watoto.


Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe

 Katika Hali Isiyo ya Kawaida Wananchi wa Kijiji Cha Igenge Kata ya Saja Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Wanaendelea Kutoa Huduma ya Kliniki Kwa Watoto Kwa Kwa Kuwaning'iniza Juu ya Miti  Kutokana na Ukosefu wa Zahanati Katika Kipindi Chote Cha Miaka 50 Ya Uhuru.

Mtandao wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com Umeshuhudia Zoezi Hilo Likifanyika Kwa Baadhi ya Wakazi wa Kijiji Hicho Ambapo Hadi Sasa Ukosefu wa Kituo Cha Kutolea Huduma ya Afya Umesababisha Kuwepo Kwa Adha Hiyo.

Wakizungumzia Tatizo Hilo Baadhi ya Wazazi wa Watoto Waliokutwa Wakiendelea na Upimaji Huo Kwa Kuning'iniza Mzani Katikati ya Mti Mmoja na Mwingine Wamesema Kuwa hadi Kufikia Kijiji Jirani Chenye Zahanati Kuna Umbali wa Takribani Kilomita Nne Hadi Tano.

Aidha Wamesema Kuwa Adha Hiyo Imekuwa Ikiwapa Shida Wananchi Katika Kijiji Hicho Hususani Kwenda
Katika Kijiji Cha Iramba Kilichopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Kupata Huduma ya Afya Kwani Tangu Kijiji Hicho Kipate Usajiri Mwaka 1995 Hakijajenga Zahanati.

Viongozi wa Kijiji Hicho Akiwemo Mwenyekiti na Kaimu Mtendaji Bwana Moshi Lugoya Wamesema Kuwa Mkakati  wa Kuwanusuru   Wananchi Hao  ni Kubadili Matumizi ya Soko Lilopo Kijijini Hapo Ili Litumike Kama Zahanati na  Kwani Tangu Lijengwe na Serikali Kupitia Mradi wa TASSAF Halifanyi Kazi Yoyote Huku Wakiendelea na Mpango wa Kuandaa Tofali Kwa ajili ya Ujenzi wa Zahanati.

Kwa Upande Wake Diwani wa Kata ya Saja Bwana Saja Bwana  Andrew Mangula amekiri kutokuwepo kwa zahanati katika vijiji hivyo Vya Igenge na Idenyimembe na Kwamba Wananchi Hao Wamekuwa Wakipata Huduma Katika Kijiji Jirani Kilichopo Mkoa wa Iringa Licha ya Kwamba Huduma Hiyo Haiwahusu Kwa Mujibu wa Bajeti Vijiji vya Kata ya saja Wilayani Wanging'ombe vinakabiliwa na changamoto mbalimbali Hali Inayowapa Wasiwasi Juu ya Karne Iliyopo na Miaka 50 ya Uhuru Iliyopo Hadi Sasa.

0 Responses to “WANANCHI WAFANYIWA HUDUMA ZA KIAFYA CHINI YA MTI WILAYANI WANGING'OMBE MKOA WA NJOMBE.”

Post a Comment

More to Read