Tuesday, July 22, 2014

WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU KATIKA BONDE LA MBWENI MPIJI


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati akitoa taarifa ya tukio la kukutwa kwa viunga vya binadamu liliyotokea jana jioni maeneo ya Bonde la Mbweni,Mpiji.



Watu wanane wanashikiliwa na polisi wakiwemo Madaktari kwa tuhuma za kuhusika kwenye tukio l a kutupwa kwa mabaki ya miili ya binadamu jana jioni nje kidogo ya jiji la Dsm

Huku likiendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametangaza kuundwa kwa jopo la upelelezi kuchunguza tukio hilo, ili kubaini taratibu gani zilikiukwa na kujua aina ya mashtaka itakayowakabili.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa miili hiyo ilikua katika Taasisi ya mafunzo ya udaktari IMTU kabla ya kukutwa imetupwa eneo la Bunju.

Taasisi hiyo imekiri kwamba mabaki ya miili ilikua katika taasisi hiyo lakini haijatoa maelezo kuhusu kutupwa kwa miili hiyo.

Kamanda Kova amewatoa wasiwasi watanzania kuwa hakuna mauaji yoyote ya kimbari yaliyotokea sehemu yeyote nchini hivyo polisi iachiwe ifanye kazi yake kisha itatoa taarifa hapo baadae.

0 Responses to “WATU WANANE WAKIWEMO MADAKTARI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA KUTUPWA VIUNGO VYA BINADAMU KATIKA BONDE LA MBWENI MPIJI ”

Post a Comment

More to Read