Thursday, August 21, 2014

MAMA AUA MTOTO WAKE KWA SUMU,NAYE AJIUA KWA SUMU,MME AAMUA KUFA KWA KUJINYONGA.

Mwanamke mmoja wa Kijiji cha Mtitu wilayani Kilolo mkoani Iringa, Grace Lubava (33), amemuua mtoto wake kwa sumu na kisha naye kujiua kwa njia hiyohiyo na baadaye mumewe, George King’ung’e (45), kujinyonga kwa kamba kutokana na vifo hivyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi na kwamba mama huyo alifariki dunia alipokuwa akipatiwa matibabu katika Zahanati ya Kilolo.
“Kifo cha mama na mtoto kilitokea baada ya mumewe kumzuia mkewe kwenda kumwona baba yake ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Tosamaganga,” alisema Mungi.
Alisema kuwa mume alimzuia mke huyo kwenda hospitali kwa madai kuwa alikuwa anakwenda kwenye mambo yake binafsi jambo ambalo lilimkera mwanamke huyo kiasi cha kufikia uamuzi huo.
Kamanda Mungi alisema baada ya King’ung’e kubaini vifo hivyo na msingi wake, aliamua kwenda porini na kujinyonga.

via>>Mwananchi

0 Responses to “ MAMA AUA MTOTO WAKE KWA SUMU,NAYE AJIUA KWA SUMU,MME AAMUA KUFA KWA KUJINYONGA.”

Post a Comment

More to Read