Thursday, August 14, 2014
MJUMBE WA NEC SHITAMBALA APANDISHWA KIZIMBANI.
Do you like this story?
Pichani ni
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) na Wakakili wa kujitegemea
Sambwee Shitambala(wa kwanza kulia) akifurahia jambo na wakili
anayemtetea Tasco Luambano mara baada ya kufikishwa katika mahakama
ya hakimu mkazi Wilaya ya Mbeya kwa shitaka la kuingia kwa jinai na
kujenga nyumba katika viwanja viwili eneo la Gombe Uyole jijini Mbeya mali ya
Jaswinder Palsigh.
Mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) na Wakakili wa kujitegemea Sambwee
Shitambala jana amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Wilaya ya Mbeya kwa
shitaka la kuingia kwa jinai na kujenga nyumba.
Mwendesha
mashitaka wakili wa serikali Ahmed Stambuli alieleza mbele ya hakimu mkazi
Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo alisema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo
kati Juni 18,2012 na Novemba 28,2013 katika eneo la Gombe Wilaya ya
Mbeya mjini.
Alisema
kuwa mshitakiwa aliingia kwa jinai katika viwanja viwili namba 27 na 28 block
BB na kujenga nyumba kinyume na kanuni kifungu cha kanuni ya
adhamu sura ya 16 ,mali ya Jaswinder Palsigh na kumsababishia mlalamikaji
maudhi.
Mshitakiwa
alikana shitaka hilo na mwendesha mashitaka alieleza mahakamani hapo kuwa
upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba upande wa mashitaka
hauna kipingamizi cha dhamana dhidi ya mshitakiwa.
Ndeuruo
alieleza mahakamani hapo kuwa dhamana ipo wazi kwa mshitakiwa kuwa na mdhamini
mmoja na kusaini bondi ya Sh1milioni ambapo mshitakiwa alitimiza masharti hayo
ya dhamana na kesi itakuwa Septemba 10,mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza
maelezo ya awali.
Akizungumza
nje ya mahakama Wakiri anayemtetea mshitakiwa huyo Tasco Luambano alisema
kuwa anashangazwa na kitendo cha kesi ya mteja wake kusikilizwa katika
mahakama ya Wilaya badala ya ardhi .
Aidha
alisema kuwa kesi hiyo inawahusu watu zaidi ya 400 “lakini cha kushangaza ni
mteja wangu pekee ndiye aliyefikishwa mahakamni hapa lazima kuna kitu ndani
yake kwani eneo analodaiwa mteja wangu kuingia kwa jinai lina nyumba za watu
zaidi ya 400 ambao wanaishi katika eneo hilo la viwanja vyote viwili”alisema
“Mteja
wangu alikamatwa jana na jeshi la polisi akiwa na watu wengine wanne ambapo
wote kwa pamoja walipewa dhamana na kutakiwa kufika hapa mahakamani
kwa ajili kusomewa mashitaka yao lakini cha ajabu wote wamefika
lakini kasomewa peke yake”
Via>Habari na matukio
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MJUMBE WA NEC SHITAMBALA APANDISHWA KIZIMBANI.”
Post a Comment