Thursday, November 27, 2014

SHEIKH WA WILAYA YA MBEYA AFA GHAFLA MAKABURINI BAADA YA KUTOA MAWAIDHA MAZISHINI




Sheikh mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini, Bakari Mketo amefariki dunia ghafla makaburini mara baada ya kuswalisha swala ya mazishi katika makaburi ya Nonde jijini na mkoani Mbeya jioni ya jana.

Sheikh huyo maarufu kwa jina la Mketo mkazi wa Nonde anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 50-60 amekutwa na mauti katika eneo la makaburi hayo ya Nonde mara tu baada ya kumaliza kutoa mawaidha kwa watu waliojumuika kumzika mama aliyefariki katika hospitali ya rufaa Mbeya juzi na msiba wake kuwekwa nyumbani kwake Sokomatola katikati ya jiji la Mbeya ambapo shekhe Mketo alitoa huduma zote tangu mwanzo wa msiba mpaka alipokutwa na mauti.

Kwa mujibu wa mashuhuda ya kifo cha sheikh Mketo waliokuwa katika makaburi hayo, wamesema kuwa marehemu Mketo hakuwa na dalili zozote za ugonjwa na wala hakulalamika kujisikia vibaya kabla ya kukutwa na mauti hayo.

Aidha mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa wakati akitoa mawaidha makaburini hapo sheikh Mketo alisisitiza sana juu ya vijana kujifunza na kuifuata vema elimu ya kiislamu na kuishika vilivyo kwani kifo hakina taarifa na akatolea mfano kuwa hata yeye anaweza kukutwa na mauti papo hapo katika eneo la makaburi na akalisisitiza hili zaidi ya mara tatu ndipo muda mfupi baadaye akadondoka na kupoteza maisha yake.

0 Responses to “SHEIKH WA WILAYA YA MBEYA AFA GHAFLA MAKABURINI BAADA YA KUTOA MAWAIDHA MAZISHINI”

Post a Comment

More to Read