fahari News
Habari | Michezo | Bishara | Zabuni
Home
BIASHARA
KITAIFA
KIMATAIFA
USA
AFRIKA
AFRIKA MASHARIKI
MICHEZO
MUZIKI
SIASA
Recommended:
Perfect Social Media Marketing Stratergy For Your Business
Like
Friday, December 5, 2014
PADRI, WENGINE WAWILI WAFA WAKIOGELEA.
Tweet
Share
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela.
Watu watatu wamekufa maji akiwamo Padri wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Same, Amedeus Mangia na wengine tisa kuokolewa baada ya kupigwa na dhoruba kali wakati wakiogelea kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu lililopo wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu Ndemanga, alisema kuwa tukio hilo limetokea juzi na kwamba watu wengine wawili waliopoteza maisha katika tukio hilo bado hawajatambuliwa majina yao.
Alisema walionusurika ni wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Chanjale kinachomilikiwa na Parokia ya Mtakatifu Stephen ya Same, ambao wote waliokolewa wakiwa hoi.
Ndemanga alisema siku ya tukio, wanafunzi hao wakiwa na mwalimu ambaye ni Padri Amedeus, walikwenda katika Bwawa la Nyumba ya Mungu kufanya hafla fupi ya kujipongeza kwa kuogelea na ghafla wakiwa majini, wimbi kubwa la maji liliwapiga na ndipo baadhi yao wakpoteza maisha.
Watu walioshuhudia tukio hilo, walisema Padri Amedeus, kabla ya kufikwa na mauti hayo aliendesha ibada katika kanisa dogo lililopo eneo la bwawani Nyumba ya Mungu.
Baba mzazi wa padri huyo, Saimon Mangi, alisema mwanaye aliopolewa na wavuvi kutoka bwawani akiwa tayari ameshafariki.
MVUA YALETA MAAFA
Katika hatua nyingine, Ndemanga ambaye pia Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya yake, alisema kuwa mtoto ambaye bado hajafahamika jina, mkazi wa kijiji cha Tolowa wilayani hapa, alipoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kuonyesha wilayani humo na maeneo mengine mkoani Kilimanjaro.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alipoulizwa alikiri pia kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi zitatolewa kwa vyombo vya habari.
(CHANZO: NIPASHE)
0 Responses to “PADRI, WENGINE WAWILI WAFA WAKIOGELEA.”
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tweets by @FahariNews
More to Read
Buzz
Twitter
Facebook
RSS
Email
Must Read
Popular Posts
MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI WA JESHI LA POLISI.
Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013 na kidato cha sita mwaka 2014 ambao w...
Nape anakupa Taarifa hii Muhimu, Kuhusu kinachoendelea kwenye Facebook yake
"Kuna acc za facebook zinasambazwa kuwasema viongozi kwa jina langu SIO ZANGU SINA ACC ZA FACEBOOK! Naamini ...
BUNGE LAINGILIA KATI SUALA LA UDA
Dar es Salaam. Wakati mjadala kuhusu umiliki wa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) ukiendelea kuwa tata, Kamati ya Bunge ya Hesa...
MKUU WA MKOA AWAASA VIJANA KUACHA ‘KUDENDEKA.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick akizindua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini. MKUU wa ...
MGONJWA WA DENGUE APATIKANA MBEYA ALAZWA HOSPITAL YA MKOA WA MBEYA.
HATIMAYE ugonjwa wa homa ya Dengue umeripotiwa kuingia Mkoani Mbeya baada ya kupatikana kwa kesi ya mgonjwa mmoja mwanamke...
0 Responses to “PADRI, WENGINE WAWILI WAFA WAKIOGELEA.”
Post a Comment