Friday, December 5, 2014
SING"ATUKI NG"O: MUGABE
Do you like this story?
Rais wa
Zimbabwe Robert Mugabe amelaumu baadhi ya watu ndani ya chama chake tawala cha
ZANU-PF kwamba wanapanga kumng'oa madarakani.
Akizungumza katika kongamano la chama hicho, Mugabe
amesema amebaini kuwepo majaribio ya kuwahonga wajumbe kumpinga kama kiongozi,
lakini akasisitiza wajumbe hawawezi kupokea hongo.
Mugabe ameahidi kupambana na rushwa ndani ya chama na
kukabiliana na maafisa wa chama hicho ambao kazi yao ni kutoa hongo na kupokea
rushwa.
Hasira ya Mugabe ilionekana kufuatia madai ya njama ya
kutaka kumuua yanayodaiwa kuandaliwa na naibu wake Joyce Mujuru. Hata hivyo
Mujuru alikanusha madai hayo ambayo yamekuwa yakimuandamana.
Mugabe alisema kutokuwepo kwa Bi Mujuru kwenye mkutano
huo wa chama kunaonyesha kuwa anaogopa.
Kadhalika Mugabe amesema Mujuru ni mwizi anayepanga
kumuondoa mamlakani kwa kushirikiana na maafisa wengine wa chama.
Chama tawala cha Zimbabwe kinakumbwa na vita vya ndani
kwa ndani kuhusiana na nani atarithi nafasi ya Mugabe ambaye ana miaka 91 na
ambaye ameongoza tangu uhuru wa taifa hilo.
Hata hivyo amekanusha madai ya kwamba anataka
kujiuzuru na kusema kuwa huo ni upuuzi.
Hivi karibuni afisa mwingine mkuu wa chama tawala,
Robert Gumbo aliiambia BBC kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amegeuza chama
tawala na kukifanya kama mali yake binafsi.
Gumbo alisema lengo kuu la Mugabe ilikuwa kuendeleza
uongozi wa chama kwa niaba ya mke wake Grace.
Bi Mujuru ambaye amekanusha madai hayo alionekana kama
mtu ambaye anechukua usukani wa chama kutoka kwa Mugabe ambaye walipigania naye
uhuru wa nchi hiyo kutoka mikononi mwa watwala wazungu.
Via>Bbc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SING"ATUKI NG"O: MUGABE”
Post a Comment