Wednesday, March 25, 2015
JUMA NYOSSO: AREJEA KUNDINI.
Do you like this story?
Emmanuel Kimbe, Katibu Mkuu wa Mcc fc |
Mlinzi wa kutumainiwa wa City Juma Nyosso anatarajia
kurejea uwanjani kutumikia timu yake kwenye mchezo wa ligi kuu ya
soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa Chamanzi Complex
mapema mwezi ujao.
Nyosso aliyekuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa michezo 8
atakamilisha kifungo hicho jumamosi ya tarehe 4.4 2015 wakati City
itakapokuwa uwanjani kucheza na Ndanda Fc kwenye mchezo mwingine wa ligi hiyo
utakaochezwa kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoni Mtwara.
Akizungumza
mapema leo Katibu Mkuu City Emmanuel Kimbe amesema kurejea kundini kwa
Nyosso kutaongeza nguvu kubwa kikosini hasa kwenye wakati huu ambao timu inafanya
jitihada za dhati kupata matokeo ili kusaka nafasi za juu kwenye msimamo wa
ligi.
“Kila mmoja hapa anayo kumbukumbu ya kazi nzuri aliyoifanya
Nyosso kwenye mechi alizocheza kabla ya kupata adhabu, niseme wazi kuwa ni
mchezaji muhimu ambaye uwepo wake unaongeza kitu, kila mmoja anaweza
kuitafsiri adhabu ile kwa namna yake, lakini uwanjani kuna mambo mengi, kuna
wakati unaweza kufanya jambo usijue ulilifanya vipi, kizuri kwetu ni kuwa
anamaliza adhabu hiyo na kurudi kuitumikia timu” alisema.
Wakati huo huo nyota wanaunda safu ya ushambuliaji Paul
Nonga, Mwegane Yeya na Themi Felix wamesema wako tayari kuwasha moto ndani ya
uwanja wa Nangwanda sijaona kwa lengo moja tu la kuipatia City
ushindi kwenye mchezo dhidi ya ndanda fc.
wakizungumza kwa nyakati tofauti nyota hao waliweka wazi kuwa
hivi sasa city iko kwenye kiwango kizuri tofauti na ilivyokuwa kwenye michezo
kadhaa iliyopita jambo ambalo kwa anamna moja ama nyingine lilikuwa
linachangia kukosekana kwa matokeo.
“Takribani
michezo mitano tuliyolicheza awali tulikuwa na matatizo kwenye kikosi wachezaji
wengi walikuwa majeruhi hiyo ilitufanya kushindwa kucheza kwenye ubora,
sasa tuko sawa na kila mmoja ana ari kubwa ya kutetea na kurudisha kile
kilichopotea, nia yetu ni kuiona city inarudi pale juu alisema Themi
Felix.
Kwa upande wao Paul Nonga na Mwegane Yeya walisema kuwa wana
uhakika City itafanya vizuri kwenye mchezo huo wa Mtwara hasa ukizingatia
matokeo mazuri yaliyopatikana uwanja wa Sokoine dhidi ya Stand United juma
lililopita.
Katika mchezo huo wa juma lililopita City iliibuka ushindi wa
mabao 2-0 yalifungwa na Yufuph Abdalah Sisalo kwa mkwaju wa penalti na Paul
Nonga aliyefunga akiunganisha krosi ya Hamad Kibopile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JUMA NYOSSO: AREJEA KUNDINI.”
Post a Comment