Monday, March 23, 2015

MZIMU WA AJALI WAZIDI KUPOTEZA MAISHA YA WATU MBEYA>>>NANE WAFA ENEO LA MAJI MAZURI.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.


WATU nane wamepoteza maisha na wengine 6 kujeruhiwa baada ya gari lenye namba za usajili T.599 AEG aina ya Fuso Mistubish kupinduka katika eneo la Maji mazuri, Wilayani Mbeya.

Tukio hilo limetokea juzi, majira ya saa mbili asubuhi katika Kijiji cha Lwanjilo Wilayani Mbeya barabara Chunya/ Mbeya.

Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Kwa upande wa majeruhi, Msangi alisema kuwa, watu sita wamejeruhiwa na kwamba wanapatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Rufaa ya Mbeya.

Kamanda Msangi ilisema, katika ajali hiyo watu saba walipoteza maisha papo hapo na mwingine wa nane aliongezeka wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Alisema, chanzo cha ajali hiyo ni kupinduka kwa Lori la mizigo ambalo lilikuwa limepakia watu na mbao likiwa katika mwendokasi eneo la maji mazuri Wilayani Mbeya kuacha njia na kupinduka.

Hata hivyo, Msangi aliongeza kuwa polisi wanaendelea na msako wa dereva wa gari hilo baada ya kufanikiwa kukimbia baada ya tukio hilo kutokea.

Wakizungumza na Fahari News katika eneo la tukio baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa lori  hilo likiwa katika mwendo kasi liliacha njia na kupinduka na kusababishaa ajali hiyo.


Amesema, Lori hilo lilikuwa limefunikwa kwa tulubai hivyo ni vigumu kwa watu au askari kubaini kwamba ndani ya gari hilo kulikuwa na abiria tofauti na bidhaa ya mbao iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Mbeya kwenda Chunya.

Mwisho

0 Responses to “MZIMU WA AJALI WAZIDI KUPOTEZA MAISHA YA WATU MBEYA>>>NANE WAFA ENEO LA MAJI MAZURI.”

Post a Comment

More to Read