Wednesday, May 13, 2015

WAUGUZI HOSPITAL YA RUFAA MBEYA WALIA NA MAGONJWA YA KUSENDEKA


Wauguzi wa Hospital ya Rufaa Mbeya wakiwa katika maandamano wakati wa kilele cha Maadhimisho ya  siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu .Picha EmanuelMadafa jamiimojablog


Wauguzi wa idara wa hospitali ya Rufaa mbeya wakifurahi jambo mara baada ya kutembelea wodi ya wagonjwa wa akili na kutoa mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa hao katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi Duniani Mei 12 mwaka huu.




Wauguzi wa hospital ya Rufaa Mbeya wakiwasha mishumaa kuungana na wauguzi wengine duninia katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka .








Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya  wakiapa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani. Wakiungana na Wauguzi wengine Duniani kuadhimishi Siku hii. 





Wauguzi wa Hospital ya Rufaa Mbeya wakiserebuka katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu sherehe ambazo zimefanyika katika ukumbi wa Romani Kathoriki jijini Mbeya





Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wauguzi duniani hospital ya Rufaa Mbeya Ndugu Joyce Komba akisoma Lisala kwa mgeni rasmi katika kuadhimisha kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu .

Wauguzi wa hospital ya Rufaa Mbeya wakimsikiliza makamu mwenyekiti wa chama cha wauguzi Hospital ya Rufaa Mbeya Ndugu Joyce Komba wakati akisoma Lisala kwa mgeni Rasmi katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wauguzi duniani Mei 12 mwaka huu ambapo sherehe hizo zilifanyika katika ukumbi wa Romani Kathoriki jijini hapa.


Makamu Mwenyekiti wa chama cha wauguzi TANNA Hospital ya Rufaa Mbeya Ndugu Joyce Komba akikabidhi Lisala kwa mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya wauguzi duninia mei 12 mwaka huu.


Katibu wa Hospital ya Rufaa Mbeya Ndugu Alinanuswe Mwansasu ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani mei 12 mwaka huu sherehe ambazo zimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa romani kathoriki jijini Mbeya.






Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA)Hospital ya Rufaa Mbeya wameitaka serikali kuhakikisha inaanzisha kitengo cha afya ya jamii kwa lengo  utoaji wa tiba kwa wagonjwa wa  maambuki ya ugonjwa wa  Kusondeka. 

Kauli hiyo imetolewa na Makamu mwenyekiti wa chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) hospitali ya Rufaa Mbeya Ndugu Joyce Robert katika kilele cha siku ya wauguzi duniani sherehe ambazo zimefanyika katika ukumbi wa romani kathoriki jijini hapa mei 12 mwaka huu .

Akisoma Lisala kwa mgeni rasmi makamu huyo mwenyekiti amesema kutokana na kuongezeka kwa magonjwa kusendeka wauguzi wamekuwa wakipata wakati mgumu namna ya kuwahudumia wagonjwa wa aina hiyo.

Hivyo amesema kuwa ili kuondokana na hali hiyo nivema serikali ikajaribu kuona uwezekano wa kuanzisha kitengo cha afya ya jamii (Public  health department)kitakacho husika moja kwamoja na utoaji huduma kwa wagonjwa wa aina hiyo  badala ya kuachiwa kwa wauguzi pekee.

Katika hatua nyingine chama hicho kimeitaka ofisi ofisi ya mkurugenzi wa hospital ya rufaa mbeya kuhakikisha inafuatilia kwa ukaribu suala la upandishwaji wa vyeo pamoja na ulipwaji wa malimbikizo yao kwa wakati .

Amesema kwa muda mrefu wauguzi wamekuwa wakipata adha kubwa kwa ufuatiliaji wa madai yao mara wanapo koma utumishi wa umma ambapo wengi wao wamekuwa wakifuatilia madai yao wizarani badala ya ofisi ya mkurugenzi hali ambayo inakatisha taama kwa watumishi hao.

Mwisho.

0 Responses to “ WAUGUZI HOSPITAL YA RUFAA MBEYA WALIA NA MAGONJWA YA KUSENDEKA”

Post a Comment

More to Read