Monday, September 28, 2015

CELINA KOMBANI KUAGWA LEO DAR


Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), Bi. Celina Kombani.

Mwili wa Marehemu Kombani ulivyoshushwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere kutoka India, juzi.


Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), Bi. 

Celina Kombani utaagwa rasmi leo Jumatatu, kuanzia majira ya saa nne asubuhi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, baada ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu na kutoa heshima za mwisho, utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro kuanzia majira ya saa tisa alasiri ambapo utalala nyumbani kwake Forest Hill.

Jumanne kuanzia majira ya saa nne asubuhi, itafanyika ibada maalum ya mazishi na baadaye mwili utaagwa katika Viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro na kufuatiwa na mazishi shambani kwake, Lukobe nje kidogo ya mji wa Morogoro.

0 Responses to “CELINA KOMBANI KUAGWA LEO DAR”

Post a Comment

More to Read