Wednesday, September 30, 2015
- IGP MANGU ATUA TARIME....ATOA UJUMBE MZITO KUHUSU UCHAGUZI
Do you like this story?
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP
Ernest Mangu amewataka Viongozi wa Vyama vya Siasa katika Wilaya za Tarime na
Rorya kufanya Kampeni za Kistaarabu ili kufanikisha Uchaguzi Mkuu pamoja na
kuimarisha Amani na Usalama Wilayani humo.
IGP Mangu aliyasema hayo wakati
alipokuwa akizungumza na Wadau wa Polisi wakiwemo Viongozi mbalimbali, Vyama
vya Siasa pamoja na Wagombea wa Viti vya Ubunge na Udiwani, wakati alipokuwa
katika Ziara ya Kikazi katika Kanda Maaalum ya Polisi Tarime na Rorya.
Alisema ili uchaguzi wa mwaka huu
uweze kufanyika kwa amani, Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea hawana budi
kuwashawishi wafuasi wao kufuata Maadili ya Uchaguzi ikiwemo kutotoleana lugha
za Matusi.
IGP Mangu alisema baada ya
Uchaguzi maisha yataendelea kama kawaida hilo ni jukumu la Wananchi wote wa
Tarime kuondoa Uhasama wao katika mambo ya Siasa kwa kuwa Siasa siyo Uhasama.
Aidha, aliwashauri Wagombea Ubunge
na Udiwani katika Majimbo ya Tarime Mjini, Vijijini, na Rorya kukutana mara kwa
mara ili kujenga kuaminiana na kutatua changamoto zinazojitokeza katika kipindi
hiki cha kampeni na hatimaye siku ya uchaguzi Mkuu.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Polisi Tarime na Rorya, kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Lazaro
Mambosasa, aliwahakikishia Wadau wote kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema
kukabiliana na vitendo vyote vya vurugu vitakavyojitokeza, pamoja na
kuhakikisha kila Mwananchi aliyejiandikisha anapata fursa ya kupiga kura bila
vitisho vya aina yoyote.
Naye Mgombea Ubunge katika Jimbo
la Rorya kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Lameck Airo alisema katika jimbo
analogombea hakuna vurugu kwa kuwa wamekuwa wakiheshimiana katika Kampeni ili
kuepusha vurugu kwa Wagombea na Wafuasi wao.
Kikao hicho kilihudhuriwa na
Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini,Vyama vya Siasa, Wafanyabiashara,
Asasi zisizo za Kiserikali, Wazee wa Kimila pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Wilaya ya Tarime.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “- IGP MANGU ATUA TARIME....ATOA UJUMBE MZITO KUHUSU UCHAGUZI”
Post a Comment