Thursday, October 15, 2015

BOBAN ATUA MBEYA CITY, AANZA KAZI YA KUIMALIZA SIMBA, LEO NI MAZOEZI SIKU YA PILI





HARUNA MOSHI 'BOBAN' AKIWA NA JUMA KASEJA AMBAYE WAMEUNGANA NAYE KWA MARA NYINGINE WAKIWA KATIKA KIKOSI CHA MBEYA CITY. WAWILI HAO WAMEWAHI KUKIPIGA PAMOJA WAKIWA SIMBA...


Boban ameanza kazi na Mbeya City na atakuwa kati ya wachezaji watakaocheza dhidi ya Simba, Jumamosi.

Leo Boban amefanya mazoezi siku ya pili mfululizo kwa ajili ya mechi hiyo.
Taarifa za uhakika zimeeleza Boban alikuwa amejiunga na Mbeya City mwanzoni mwa msimu huu.
Lakini kulikuwa na mambo kadhaa aliyotakiwa kumalizana na uongozi wa timu kabla ya kujiunga nayo.

Taarifa nyingine zimeeleza Boban alisafiri kwenda kufanya majaribio nje ya nchi.

0 Responses to “BOBAN ATUA MBEYA CITY, AANZA KAZI YA KUIMALIZA SIMBA, LEO NI MAZOEZI SIKU YA PILI”

Post a Comment

More to Read