Saturday, October 17, 2015

WANANCHI WADAIWA VITAMBULISHO VYA KURA KWA LAZIMA MOROGORO





Ikiwa imebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu katika hali isiyo ya kawaida watu wanne wasiofahamika itikadi zao za kisiasa wame kamatwa na wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo(Chadema) kwa madai ya kupita katika kata za manispaa ya Morogoro na kudai shahada za wapiga kura kwa nguvu na kuanza kuorodhesha majina ya wananchi na namba zao za simu.

Wakizungumza baada ya kuwafikisha watu hao katika kituo cha polisi viongozi wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Morogoro Jemsi Mkude wamesema watu hao walikuwa wakiwalaghai wananchi kwa kuandikisha vyama vyao vya siasa, namba zao za shahada za kupigia kura, namba zao za simu pamoja na kero zinazowakabili kwenye eneo hilo ambapo wamelitaka jeshi la polisi kutenda haki ilikuepusha uvunjifu wa amani.

Kwa upande wananchi mashuhududa walio kumbana na watu hao katika harakati za kuwaandikisha wapiga kura majina wameeleza jinsi watu hao walivyokuwa wakifanya zoezi hilo kwa kudai kwa lazimima shahada za kupigia kura ambapo baadhi ya watu walikubali na wengine waifa kwa afisa mtendaji wakata na wananchi waliamua kuungana na kuwatia hatiani na kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi cha mji wa Morogoro.

Akitolea ufafanuzi kuhusiana na suala hilo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Morogoro mjini Bi Theresia Mahongo amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai na kwamba adhabu yake ni faini kati ya shilingi laki moja hadi laki mbili au kifungo cha miaka miwili ama vyote na kuwaonya wananchi kuacha kufanya hivyo nikosa la jinai.

Chanzo:ITV Habari

0 Responses to “ WANANCHI WADAIWA VITAMBULISHO VYA KURA KWA LAZIMA MOROGORO”

Post a Comment

More to Read