Monday, November 9, 2015
HASSANI KESSY BADO ANAMKATABA NA SIMBA.
Do you like this story?
![]() |
Nyota ya beki wa pembeni wa klabu ya Simba SC Hassan Ramadhani Kessy |
Nyota ya beki wa pembeni wa klabu ya Simba SC Hassan Ramadhani Kessy
inazidi kung’aa ikiwa ni siku kadhaa tu toka aitwe kwa mara ya kwanza katika
katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania
Taifa Stars, tayari ametajwa kuhitajika na mahasimu wa jadi wa Simba klabu ya Dar Es Salaam Young African.
Jumapili ya November 8 magazeti kadhaa ya
bongo yaliandika kuhusu beki huyo kuwa na uwezekano wa asilimia 75 ya kujiunga
na klabu ya Yanga
licha ya kuwa mkataba wake bado na Simba
haujawekwa wazi unaisha lini. Hassan
Kessy kwa sasa yupo Johannesuburg
Afrika Kusini na anatajwa kujiunga na Yanga
mara atakaporejea Dar Es
Salaam. Hizo zilikuwa headlines kutoka katika magazeti ila
hii ni kauli ya afisa habari wa
Simba Haji Manara.
“Mashabiki wa Simba niwaambie kitu kimoja
Kessy bado ana mkataba na Simba, Kessy akisharudi kambi ya timu ya taifa kutoka
Afrika Kusini tutafanya nae mazungumzo na ataongezewa mkataba kwa sababu kocha
wa Simba Dylan Kerr na viongozi bado wana mipango na Kessy, hivyo Kessy ana
mkataba na Simba na hatokwenda klabu yoyote” >>> Haji Manara
Hata hivyo kuna dalili za beki huyo kukaribia
kusajiliwa na Yanga
hususani tukiwa tunaelekea katika kuanza kwa dirisha dogo la usajili zinapata
uzito, kwani kauli ya Haji
Manara kuwa akirudi Kessy
ataongezewa mkataba kitu ambacho kinadhihirisha mkataba wa beki huyo kuwa
umebakiza miezi sita hivyo kisheria Yanga
wanaruhusiwa kuzungumza na Kessy
bila kuwahusisha Simba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HASSANI KESSY BADO ANAMKATABA NA SIMBA.”
Post a Comment