Monday, April 18, 2016
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO LEO
Do you like this story?
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru kwenye Uwanja
wa Jamhuri Mkoani Morogoro leo.
Katika uzinduzi
huo, Makamu wa Rais alimnukuu Baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere akisema kuwa
nia ya Mwenge wa Uhuru tangu mwanzo ni kumulika mipaka ya nchi yetu dhidi ya
maadui, kuleta matumaini pale ambapo hakuna matumaini, kuondoa chuki pale
ambapo kuna chuki na kuleta heshima pale ambapo kuna dharau.
Alisema
nia hiyo ya kuwepo kwa Mwenge wa Uhuru kama alivyomnukuu Baba wa Taifa,
inaendana na dhana ya kutumbua majipu katika Serikali ya awamu ya tano. Alisema
utumbuaji majipu unalenga kuleta matumaini kwa wananchi ambao wamekata tamaa na
kuleta heshima kwa wananchi waliodharauliwa.
“Kaulimbiu
ya mbio ya za mwenge mwaka huu ni hii: Vijana ni nguvu kazi ya taifa,
washirikishwe na wawezeshwe,”alisema
Makamu wa Rais na kuongeza kuwa vijana ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa
hawajatumika ipasavyo kutokana na sababu mbalimbali.
Alizitaja
baadhi ya sababu au changamoto zinazowakabili vijana nchini kuwa ni ukosefu wa
ajira, uwezo mdogo wa kuajiri kwenye soko la ajira, ukosefu wa mitaji rafiki
kwa vijana, maeneo ya kufanyia kazi pamoja na mitazamo hasi kwa baadhi ya
vijana kwa kuchagua kazi.
Makamu wa
Rais pia amewataadharisha vijana kutokana na ongezeko kubwa la maambukizi ya
ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya.
Amesema
vijana wenye umri kati ya miaka 16-24 ndiyo wanaongoza kwa kuathiriwa na
maambukizi ya ukimwi.
Amesema
athari za ukimwi na madawa ya kulevya kwa vijana ni kubwa lakini pia zinaongeza
mzigo kwa jamii na serikali katika kuwatibu, kuwahudumia na kuongezeka kwa
vifo.
Kwa upande
wake, Waziri Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama, amemtambulisha
George Jackson Kijimba kuwa ndiye kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu
akisaidiana na wakimbiza mwenge wengine watano.
Alisema
sherehe za kuhitimisha mbio hizo za mwenge wa uhuru zitafanyika mkoani Simiyu
tarehe 14 Oktoba mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOANI MOROGORO LEO”
Post a Comment