Thursday, April 27, 2017
Young Africans Kuondoka Dar es salaam Leo
Do you like this story?
Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Young Africans
kitaondoka jijini Dar es salaam leo jioni kuelekea Mwanza kwa ajili ya
mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho (Azam Sport Confedaration
Cup).
Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi utaondoka saa 11 jioni na ndege ya shirika la ndege la ATC.
Wachezaji watakao ondoka ni Makipa: Deogratius Munishi ,Beno
Kakolanya na Ally Mustapha. Nafasi ya ulinzi ni Nadir Haroub,Vicent
Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin
Yondani.
Nafasi ya viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deusi
Kaseke,Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimoni Msuva, Geofrey Mwashuiya na
Emmanuel Martin.
Upande wa washambuliaji ni Amissi Tambwe , Matheo Antony na Obrey Chirwa.
Wachezaji watakaoukosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ni Malimi Busungu, Vincent Bossou na Donald Ngoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Young Africans Kuondoka Dar es salaam Leo”
Post a Comment