Sunday, August 27, 2017
Wachezaji wa Taifa Stars walioitwa kambini kujiwinda na Botswana
Do you like this story?
Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’,
Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Botswana katika
mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu
Agosti 28 hadi Septemba 2, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza
Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2,
2017.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya
Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya
Tanzania wakiwa ni saba akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kinachotarajia kuingia kambini kesho Jumapili kuanzia
saa 2.00 usiku ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na
Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi
ni Gadiel Michael (Young Afric
ans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda
(Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba
SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo
ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya),
Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El
Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania)
na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana
Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni
Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa
Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt.
Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “Wachezaji wa Taifa Stars walioitwa kambini kujiwinda na Botswana”
Post a Comment