Wednesday, September 13, 2017

Petr Cech awataka wenzake kupambana kama Chelsea


Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech, ambaye aliwahi kutwaa ubingwa wa Europa league akiwa na Chelsea, amewataka wachezaji wenzake kupambana kufa na kupona ili kufanikisha mpango wa kufanya vyema kupitia michuano hiyo ya barani Ulaya.
Amesema: “Tunapaswa kuchukua maamuzi ya kupambana kwa vyovyote vile, ili tufikie lengo.
“Nilipokua Chelsea, kila mmoja wetu alisikitishwa na hatua ya kutolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi, lakini tulipoanza kushiriki Europa League kila mmoja alijitoa kwa hiyari yake na tukafanikiwa kutwaa ubingwa, ninaamini suala hilo linawezekana nikiwa Arsenal.
“Jambo kubwa ni kujikubali na kutambua unapambana kwa lengo la kufanya vyema, nimeshawahamasisha wenzangu kwa kutaka kuona suala hilo linatokea ili iwe furaha kwetu sote mwishoni mwa msimu.”
Arsenal wanashiriki michuano ya Europa League, kutokana na kumaliza katika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ya nchini England msimu wa 2016/17.

0 Responses to “Petr Cech awataka wenzake kupambana kama Chelsea”

Post a Comment

More to Read