Wednesday, September 13, 2017

Serikali kununua mashine za DNA


Serikali imedhamiria kununua mashine tatu za vipimo vya vinasaba (DNA) ili zitumike katika maabara za Kanda na hivyo kusogeza huduma karibu na wananchi.
 
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Dkt. Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Chumbuni, Ussy Pondeza kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya uchunguzi wa sampuli ikiwemo sampuli za makosa ya jinai.
 
Amesema kuwa Serikali ina mkakati wa kuongeza mashine hizo ili kuwezesha uchunguzi kufanyika kwa wakati kwa vielelezo vya makosa ya jinai ikiwa ni pamoja na vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto.
 
” Sampuli za uhalali wa watoto kwa wazazi zinafanyika kwa wepesi zaidi kuliko sampuli za makosa ya jinai kwani sampuli hizo zinachukuliwa moja kwa moja toka kwa wahusika hivyo kurahisisha uchunguzi wake endapo wahusika wa uchukuaji watachukua kwa umahiri na uhifadhi utafanyika kwa namna stahili,” amesema Dkt. Kigwangala.
 
Aidha, amesema kuwa sampuli za uchunguzi wa makosa ya jinai zinachukuliwa toka maeneo ya matukio hivyo uchunguzi wake unaweza kuchukua muda zaidi kutegemeana na aina ya sampuli na eneo zilipotoka.

 
Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali inampango wa kuanzisha kituo cha kupima vinasaba (DNA) Mkoani Mbeya kwa lengo la kupunguza ucheleweshaji wa matokeo ya uchunguzi

0 Responses to “Serikali kununua mashine za DNA”

Post a Comment

More to Read