Monday, June 23, 2014
MKOA WA MBEYA WASAIDIWA NA SERIKALI YA WATU WA MAREKANI.
Do you like this story?
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro akitoa wito kwa viongozi wa Wilaya zilizopata Magari |
Katibu wa Hopitali ya Mkoa wa Mbeya Bi Juliana Mawaka akitoa taarifa katika kukabidhi Magari ya VVU/UKIMWI Mbeya |
Picha ya Magari yaliyo kabidhiwa |
Serikali
ya Marekani kupitia Mradi Walter Reed Program imetoa msaada wa
magari Matatu kwa uongozi wa serikali ya Mkoa wa Mbeya yenye thamani ya
shilingi mil400.3.
Magari
hayo yamekabidhiwa leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, kutoka kwa
mwakilishi wa Shirika la Walter Reed Tanzania Daktari Joseph
Chintowa.
Akipokea
msaada huo, Kandoro amesema magari hayo yamefika kwa muda muafaka lakini jamii
inapaswa kutambua kuwa misaada hiyo haipunguzi ongozeko la magonjwa ya ukimwi
pamoja na saratani.
Misaada
hii haipunguzi ongezeko la magonjwa ni lazima tudhibiti tamaa ya mwili,
tusijidekeze kwenye vitendo vinavyotuingiza kwenye ngono zembe,
Akitoa
neno mara baada ya kukabidhi magari hayo Dokta Chintowa, amesema shirika la
Walter Reed limekuwa likifanya kazi kwa miaka kumi sasa kwa niaba
ya wizara ya afya ustawi wa jamii katika kusaidia utekelezaji wa
mpango wa udhibiti wa ukimwi kwa mikoa ya Mbeya,Rukwa na Ruvuma.
Amesema
mpango huo umekuwa ukipitia katika mfuko maalumu wa Rais wa
marekani wa PEPFAR ambao umekuwa ukitoa msaada wa kuzuia
maambukizi ya ukimwi kutoa huduma za uangalizi na
ufuatiliaji wa ukimwi.
Aidha
mwakilishi huyo amebainisha kuwa sanjali na hayo pia mfuko huo umekuwa
ikisaidia mikoa hiyo pamoja na mingine ya Tanzania katika
kuzijengea uwezo idara za afya na jamii kwa ujumla katika mapambano
hayo dhidi ya ukkimwi.
Amesema
magari hayo yatatumika katika kuendeleza na kuboresha
harakati za serikali dhidi ya ukimwi pamoja na mradi mpya wa
HJFMRI,WRP unasaidia katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na vitendo
viovu dhidi ya watoto.
Amesema
Takwimu ziaonyesha kuwa pamoja maambukizi ya kimokoa kuwa juu kwa
asilimia 9.0 pamoja na vitendo vya ukatili kuwa hivyo katika msaada wa
magari hayo matatu moja kati hayo litatumika katika mradi wa kupambana na
vitendo vya ukatili wa kijinsia ambapo mengine yatapelekwa katika Halmashauri
ya Busokelo na Momba kwa lengo la kuzijengea uwezo Halmashauri hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MKOA WA MBEYA WASAIDIWA NA SERIKALI YA WATU WA MAREKANI.”
Post a Comment