Wednesday, August 27, 2014
CHINA YAIMWAGIA MISAADA JESHI LA POLISI, NAIBU WAZIRI SILIMA ATOA PONGEZI.
Do you like this story?
Na. Tamimu
Adam – Jeshi la Polisi
Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi imekabidhiwa msaada wa vifaa vyenye thamani zaidi ya
milioni mia moja kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa ajili ya
matumzi ya ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya ndani na ukumbi wa mikutano
wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Msaada huo,
ulitokana na Ziara ya Naibu Waziri wa Usalama wa raia wa Jamhuri ya watu China
aliyoifanya hapa nchini mwezi mei mwaka jana ambapo aliahidi misaada mbalimbali
kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Polisi.
Miongoni mwa
vifaa vilivyokabidhiwa na Balozi wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe.
Xu Youqing kwa Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima ni
pamoja na Kompyuta Thelasini (30), Viti tisini na mbili (92), Meza hamsini (50)
na PA System kwa ajili ya kumbi mbili za mikutano.
Aidha, Balozi
wa Jamhuri ya watu wa China hapa nchini Mhe. Xu Youqing alikabidhi Pikipiki
hamsini (50) kwa Jeshi la Polisi ambazo zilipokelewa rasmi na Naibu
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima. Pikipiki hizo zilitolewa
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China kwa niaba ya jumuiya ya
wafanyabiashara wa kichina walipo Afrika wakati wa ziara yake aliyoifanya hapa
nchini mwezi juni mwaka huu.
Kwa upande
wake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Pereira Silima baada ya kupokea
vifaa hivyo, alimshukuru Balozi huyo wa China na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa
China Pamoja na Wafanyabiashara wa Kichina waliopo Afrika kwa msaada walioutoa
kwa Serikali ya Tanzania, na kueleza kuwa vifaa hivyo vyote vitakuwa ni chachu
katika kuzuia, kupambana na kukabiliana na uhalifu hapa nchini.
Naye, Naibu
Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki alisema kuwa mbinu za kutenda
uhalifu hubadilika mara kwa mara kulingana na mabadiliko ya kiteknolojia, na
katika kukabiliana na mabadiliko hayo Jeshi la Polisi liko kwenye utekelezaji
wa Maboresho yaliyojikita katika mihimili mikuu mitatu ambayo ni kulifanya
Jeshi kuwa kisasa, lenye weledi na linaloshirikiana na wananchi katika
kukabiliana na vitendo vya uhalifu, hivyo vifaa vilivyokabidhiwa vitalisaidia
Jeshi la Polisi katika mpango huo unaolenga kuzuia uhalifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CHINA YAIMWAGIA MISAADA JESHI LA POLISI, NAIBU WAZIRI SILIMA ATOA PONGEZI.”
Post a Comment