Wednesday, September 3, 2014
TAMKO LA JESHI LA POLISI
Do you like this story?
![]() |
JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri. |
Akizungumza
Dar es Salaam, Septemba 3,2014 Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema
kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu
tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.
“Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya
watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo
yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua viongozi wa
Serikali.
“Wengine wamekuwa
wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina,
ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria
haitamuacha, amesema.
Senso aliendelea kubainisha
kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa
hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria
au la, atachukuliwa adhabu kali.
Alisema oparesheni ya
kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina hiyo.
Aliongeza kuwa hatua hiyo
pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na kujipatia
kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs zinazosambaza picha chafu
ambazo ni kinyume na maadili.
“Wapo baadhi ya watu wanatumia
mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya
waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake,” amesema.
Hivyo alisisitiza kuwa
Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka
wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.
Pia aliziomba kampuni za
simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo wasiruhusu uende kwa
mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAMKO LA JESHI LA POLISI”
Post a Comment