Tuesday, July 26, 2016

TANZANIA PRISONS YAENDELEA KUJIFUA ZAIDI KUELEKEA LIGI KUU TANZANIA BARA.MBEYA


Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons (Meja Mstaafu) Abdul Mingange akitoa maelezo kwa wachezaji mara baada ya kumaliza mazoezi.



Wachezaji wa Prisons wakiwa katika Mazoezi kujiandaa na Ligi Kuu.


Wachezaji wa Prisons wakiwa katika Mazoezi kujiandaa na Ligi Kuu.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons (Meja Mstaafu) Abdul Mingange akitoa maelekezo kwa Mchezaji Meshack.

TIMU ya soka ya Tanzania Prisons ya jijini hapa imeendelea kukisuka kikosi chake kwa jili ya msimu wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimua vumbi Agosti mwaka huu baada kusajili makinda nane wasio na majini kutoka timu mbalimbali hapa nchni.

Akizungumza na Fahari New  Meneja wa timu Tanzania Prisons Enock Lupyuto alisema kuwa wacheazji hao si wale wenye majina makubwa lakini wanuwezo wa kusakata soka.

Lupyuto alisema kuwa wachezaji hao wamesajiliwa baada kufanyia kazi  mapendekezo yalitolewa na kocha aliyeondoka Salum Mayanga ambaye ameenda kukinoa kikosi cha Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro.

Amesema kuwa wachezaji hao wapya, watano wametoka ligi daraja la kwanza na ligi kuu huku wachezaji wawili wakipandishwa kutoka kikosi cha ‘Under 20’ na mmoja ni askari Magereza ambaye amahamishwa kutoka Mkoa wa Mwanza.

Hata hivyo akizungumzia wachezaji hao wapya, kocha msaidizi Shabani Kavumba alibanisha wachezaji hao na vilabu walivyo toka kuwa ni Afrikan Sport,Mgambo Shooting,Kagera Sugar, huku akieleza kuwa hawawezi kuweka wazi majina yao mpaka pale shirikisho la mpira wa Miguu nchini TFF litakapofungua rasmi dirisha la usajili.
Mwisho

0 Responses to “TANZANIA PRISONS YAENDELEA KUJIFUA ZAIDI KUELEKEA LIGI KUU TANZANIA BARA.MBEYA”

Post a Comment

More to Read