Saturday, August 6, 2016
SIMBA YAWASAINISHA MIKATABA WACHEZAJI WATANO WA KIGENI
Do you like this story?
Method Mwanjali (katikati) akisaini Mkataba wa kujiunga na Simba SC leo |
Rais wa Simba, Evans Aveva (kushoto) akimkabidhi Laudit Mavugo (kulia) jezi ya Simba baada ya kusaini |
Bokungu (katikati) akisaini Mkataba wa kuitumikia Simba SC. |
Blagnon (katikati) akisaini Mkataba wa Simba SC. Kulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Collin Frisch na kushoto Rais wa klabu, Evans Aveva |
Klabu
ya Simba yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es Salaam leo
imekamilisha usajili wa wachezaji wake 5 ili kukiongezea nguvu kikosi chake.
Aveva
amewataja wachezaji hao kuwa ni pamoja na mabeki Janvier Besala Bokungu kutoka
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Method Mwanjali kutoka Zimbabwe, kiungo
Mussa Ndusha kutoka DRC pia na washambuliaji Frederick Blagnon kutoka Ivory
Coast na Laudit Mavugo wa Burundi.
Usajili
huo wa mchezaji Laudit Mavugo ambaye wapenzi na wanachama wengi wa Simba
wamekuwa wakimsubiri Kwa hamu.
Fahari
News iliongea na Rais wa Simba Evans Aveva baada ya usajili huo kumalizika
ambapo alisema
"ni
jukumu lete sisi kama viongozi kuhakikisha tunatimimza matakwa na mahitaji ya
benchi letu la ufundi ambapo baada ya muda wa wachezaji hawa kufanya majaribio
wakiwa kambini Morogoro na benchi la ufundi kujiridhishe kuwa wanafaa kuwa
katika kikosi chetu, leo walimalizia na vipimo vya afya na hapa ndio wakasaini
mikataba rasmi kuitumikia klabu ya Simba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SIMBA YAWASAINISHA MIKATABA WACHEZAJI WATANO WA KIGENI”
Post a Comment