Tuesday, February 25, 2014


CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO WANAFUNZI WA KIKE


Kwa mujibu wa serikali,zaidi ya wanafunzi 8000 wanaacha masomo kwa kupata ujauzito kila mwaka. baadhi ya sababu za ujauzito serikali inasema ni pamoja na mila zinazochochea  ndoa za utotoni,wasichana kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji kama ubakaji,tamaa za wanafunzi wenyewe,maisha duni ya familia na wanafunzi kusafiri umbali mrefu wakati wa kwenda na kurudi shule.

Pamoja na mikakati iliyopo ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu ,hali halisi katika maeneo mengi nchini inaonesha kuwa bado kuna vikwazo mbalimbali vinavyowazuia wasichana kupata haki hiyo ya msingi.

kwa mfano mara kwa mara wadau wa elimu kupitia ripoti zao wamekuwa wakisema watoto wakike nchini wakiwemo wanafunzi hawako salama.

wanafunzi hao ni waathirika wakubwa wa vitendo mbalimbali vya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa . Ukweli ni kwamba wanafunzi wakike hawako salama nyumbani, njiani wanapoelekea au kurudi shule na hata shuleni kwenyewe.

0 Responses to “ ”

Post a Comment

More to Read