Tuesday, February 25, 2014
Do you like this story?
MISRI KUNANI BARAZA LA MAWAZIRI?

Waziri mkuu wa Misri, Hazem el-Beblawi na baraza lake la mawaziri wamejiuzulu.
Bwana El-Beblawi alisema kuwa Misri imeshuhudia ongezeko la
migomo katika sekta ya umma katika wiki chache zilizopita.
Alisema kuwa hakuna hata serikali moja duniani ambayo inaweza kutimiza mahitaji ya watu wake katika kipindi kifupi sana.
Serikali hiyo ya mpito ilianza kazi mwezi Julai mwaka jana baada ya jeshi kumpindua aliyekuwa Rais Mohammed Mosri
Taarifa zinasema kuwa uamuzi wa baraza la
mawaziri kujiuulu ulitokea baada ya mkutano kati ya mkuu wa majeshi na
waziri wa ulinzi Field Marshal Abdul Fattah al-Sisi.
Inataarifiwa kuwa al-Sisi anatarajiwa kujiuzulu kutoka katika wadhifa wake ili kugombea Urais.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ”
Post a Comment