Sunday, February 23, 2014
Do you like this story?
TUTU AMSIHI MUSEVENI KUHUSU MSWADA WA NDOA ZA JINSIA MOJA

Askofu mstaafu wa Cape Town, Desmond Tutu, amemsihi Rais
Museveni wa Uganda asitie saini mswada ulioleta utatanishi kuhusu wapenzi wa
jinsia moja.
Askofu Tutu, aliyewahi kupata tuzo ya amani ya Nobel, alisema amevunjika moyo kuwa Rais Yoweri Museveni anaonesha kubadilisha msimamo wake, kwa vile awali alisema kuwa hataruhusu mswada huo kuwa sharia.
Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani.
Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa.
Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ”
Post a Comment